Wataalamu wa ardhi waweka mikakati ya kuongeza urasimishaji ardhi Urambo

Wataalamu wa ardhi waweka mikakati ya kuongeza urasimishaji ardhi Urambo

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
3a6b1a6f-675e-47b8-9f5c-797c3190fdc6.jpeg

TABORA: Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Tabora, Bw. Tumaini Gwakisa, akiambatana na wataalamu wa ardhi, akiwemo Msajili Msaidizi wa Hati Mkoa wa Tabora Na.Samweli Ibrahimu na Msajili Msaidizi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa Mkoa wa Tabora Bw.Franklin Chonjo,wamekutana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Bi. Grace Quinteen, tarehe 1 Oktoba 2026, katika ofisi yake.

Mkutano huo ulilenga kujadili na kuweka mikakati ya kuongeza na kuharakisha urasimishaji wa ardhi kwa wananchi, pamoja na kuimarisha utatuzi wa changamoto mbalimbali za ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na Mkoa wa Tabora kwa ujumla.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata usalama wa miliki za ardhi, huduma bora na suluhu za changamoto za ardhi kwa ufanisi zaidi.
 
Shida urasimishaji ni gharama mno,bila kuanzia milioni 3 huwezi kupima hadi kupata hati,tena hasa dar!
 
Back
Top Bottom