Wataalamu wa kilimo naombeni msaada

Wataalamu wa kilimo naombeni msaada

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Mzazi wangu kalima matikiti hekari 5. Ni kilimo cha umwagiliaji. Hakushirikisha mtu yoyote. Kulima, kununua mbegu, gharama za mafuta kuvutia maji katumia zaidi ya 20,000,000. Na ni Mara ya kwanza kulima matikiti.

Anasema anategemea kupata faida. Sisi wanae hatujaridhika na uamuzi huo maana kilimo na kamari. Kwa sasa haelewi mtu. Hivi mnaolima mnatupa fedha zote hizo ardhini?
 
Mwanbia bora abet mechi ya Yanga na wale wasudan amuue yanga atapiga hela.

Mzee anakaribisha magonjwa ya presha, sukari, figo, ini na hatimae kifo.
 
Nimeongea nae anasema hela sio zangu nitafute zangu, angalau angeanza na walau 5,000,000.
 
Cha muhimu mwache aje akutane mwenyewe na matokeo ya kile anachokifanya.
 
Mnaolima mnafanya haya wadau kufukia kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo, tumesikitika sana, japo hela sio zetu inauma mzazi anafukia kiasi kikubwa cha pesa kwenye udongo.
 
KAKA USIMKATISHE TAMAA, HATA TIKITI ZINALIPA SANA TU ILA KWA BAJETI HIYO MSHAURI ALIME NYANYA. NHEE MKUU UTAKUJA NISHUKURU.
 
KAKA USIMKATISHE TAMAA,HATA TIKITI ZINALIPA SANA TU...ILA KWA BAJETI HIYO MSHAURI ALIME NYANYA..NHEE MKUU UTAKUJA NISHUKURU..
Ameshalima hayo matikiti
 
KAKA USIMKATISHE TAMAA,HATA TIKITI ZINALIPA SANA TU...ILA KWA BAJETI HIYO MSHAURI ALIME NYANYA..NHEE MKUU UTAKUJA NISHUKURU.
Nina hofu kubwa mkuu kwamba atarudisha hizo fedha mkuu,najua hasara zipo ila mkuu kiasi hicho no kikubwa kwa mwanzaji na hana experience na kilimo hicho na anaulizia tu wakulima wengine.
 
Nina hofu kubwa mkuu kwamba atarudisha hizo fedha mkuu,najua hasara zipo ila mkuu kiasi hicho no kikubwa kwa mwanzaji na hana experience na kilimo hicho na anaulizia tu wakulima wengine
Kilimo kinategemea sana lini unavuna ili kupunguza risk ya hasara alime matikiti,nyanya na hoho/carots ili asikose kote
 
Hapo ungeweka picha na maelezo ya hayo matikiti yana muda gani toka aanze kulima.

Ingesaidia kujua kama hiyo hela itarud au la.
 
Back
Top Bottom