Wataalamu wa lugha ya kingereza msaada kwenye tuta

Wataalamu wa lugha ya kingereza msaada kwenye tuta

post imekaa kimzaha mzaha lakini kupitia kwayo kuna mengi tumejianika. hata sisi wakosoaji/wasomaji tumejianika (idadi yetu) si haba lugha iliyoletwa na ngalawa inatushika. shukurani kwenu magwiji wenye uthubutu mmetunoa.

japo sitaki kuamini maneno ya OP kuwa ni kazi iliyomhusisha mwalimu; sikufunzwa kumtweza mwenye nafasi yake na hususani kama ndiko anajipatia ugali wa kila siku. nabaki kuamini ni kazi ya mhuni mmoja tu kapenda kuzichangamsha akili zetu ili ras nanii ajitwalie utukufu. mwalimu apewe maua yake wametutoa mbali wakiwa katika mazingira magumu. heko mwl. Bulakokoye mukagunda 1994-95 kula uzee wako. wakagakoze mtama

hoja kuntu hapa ni; lolote kwa sera za sadikika linawezekana. tangu enzi tunakuzwa mwanafunzi bora hujulikana kwa ufaulu wa mitihani-nilisikia kwamba hadi hesabu zilipata kuingizwa katika majibu ya kubashiri)kuchagua! Ajabu. ile ladha ya kuchora jedwali la Swali/kazi/jibu wataalam hawakuona umuhimu wake.

huko sekondari aliyepata daraja la I na II (kwa tafsiri yao amefaulu vizuri( anaenda kusoma kidato 5 na 6. wale wa daraja 3, 4 nasikia mliwahi kuambiwa na 5 pia (ufaulu hafifu) wanasukumwa vyuo na kutemgeneza wataalam wa 'have' na 'has'.

yaani umechukua dumu la petrol ukamwagia nyumba, ukawasha njiti; nyumba inateketea bado urudi kushangaa imekuwaje ikateketea! sasa hapo ajabu iko wapi?

"HAS" na "HAVE" hata sio wa mabasi ya njano. tuliosoma Mr. Daudi, Mrs Daudi, Musa, Neema and Baraka; kitabu amazing landscap cha kijani hapa najua tunacheka.

nb. mchina hazingatii vyeti, bali unachokitoa akilini kuumba kinachoshikika/tumika na wengi. hata kihangaza ni lugha muhimu kikubwa ikidhi hitaji la mawasiliano.
 
Back
Top Bottom