Wataalamu wa madini, naweza kununua haya mawe kwa shilingi ngapi na kupata faida?

Haya huna haja ya kununua..unapewa tu bure. We usipende kila kitu kutaka kununua. Hayo yapo mengi tu huko wanakoyatoa.
 
Hivi vidubwasha sivifahamu hata kidogo
 
Haya si zaidi ya kilo mbili hiyo ni pesa ndefu sana kama ni yenyewe
 
Mkuu japo wanasema kila biashara ina mwanzo wake na kujifunza kwake ila nenda taratibu! Iwapo hata a b c ndogo kabisa za biashara hii huna unauliza hapa mkuu jiandae kutoa sadaka za kutosha tu.
 
Nimegoogle ni hela ndefu,, gram 20, inakwenda hadi 1.2 M.
Nje ya dhahabu gram tu haidetermine bei ya madini. Ukubwa wa madini, mng'ao wake na quality ni jambo muhimu katika madini mengine. Yani unaweza nunua mfano ruby kipande cha ukubwa flani chenye carat kadhaa kwa pesa nyng sana halafu ukanunua ruby vipande vya ruby vidogo vidogo vingi vyenye uzito zaidi ya hiyo kwa bei ya kutupa.
 
Poor tourmaline bicolor hata bure usichukue utajaza uchafu nyumbani
 
Mkuu hio ni green tourmaline ingawa naona quality yake ni very poor. Kwa quality hiyo km una nia yakununua bas yachukue kwa bei ya kg na sio kwa grams. Lakin kabla yakununua hem chek ofis ya madin ilio karibu nawe upate update ya Bei ilio sokon au pia wanakuaga na buyers wakakuunganisha.

Option nyingine, chukua vipisi kadhaa Kama sample (bila kulipia)then nenda mitaa ya Morocco dsm pale hua Kuna wahindi wananunua kwa kgs, watakupa Bei ya soko.
 
Aisee asante sana umeniokoa mzee, So kulitambua jiwe Pure natakiwa nizingatie nini wakati wa kulikagua? Pia Nitashukuru Sana Ukiniambia bei ya kilo kulingana na hayo unayoyaona hapo naweza kununua kwa kiasi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…