Wataalamu wa mambo ya madini

Wataalamu wa mambo ya madini

Kuna biashara yenye uhakika wa mafanikio 100%? Kama ipo bora ufanye hiyo.

Uchimbaji ni kama biashara zingine zote basics ni zile zile hakuna kitu kipya. Uwe na eneo lenye deposits ya hayo madini, vibali, vifaa, utaalam na mtaji. No more, no less.
Kwasisi wafanyabiashara zipo biashara zenye uhakika wa mafanikio...kwa comment uliyoweka inaonyesha kabisa haujawahi kufanya biashara yeyote
 
Sijawahi kufanya biashara ndo maana mleta uzi kanitag specifically.

Fanya hiyo biashara yenye uhakika achana na madini.
 
Mkuu unataka kufahamu kuhusu nn? Bei ya crusher au unataka kujua kama crusher mashines zinatengenezwa hapa hapa bongo?

Nyooka vizuri tukusaidie.
Mkuu Dexta,
Asante sana, nilihitaji kufahamu bei ya karasha pamoja na vibali kuanzia ngapi ya kwanza kama vile unaelekeza begineer.
Na hizi karasha process zake inakuaje

Ahsante
 
Crusher/karasha zinaanzia 8m-15m kutegemeana na ubora wa plates zake. Si vyema sana kuanza hizi harakati kwa kununua hizi Crusher bila ya kuwa na uhakika wa kupata mawe. Na siyo mawe/ore tu bali mawe(ore) inayosoma vizuri. Naposema kusoma namaanisha kiwango cha Dhahabu(PPM) kilichomo kwenye mawe hayo.
Ni bora zaidi kabla hujafungua mwalo (Prossesing plant) huwe na shimo au mashimo ya uhakika ya kukupatia mzigo yaani ore. Mashimo aya yanaweza kuwa yako au ya watu ukaingia nao share.

Mtaji wa kuanza nao! Inategemea unataka nini lakin tambua Uchimbaji ni gharama sana haswa vifaa vyake. Mfano ili Upate Mwalo wa kawaida unahitaji mashine kama Jaw crusher(up to 9m), Ball mill(karasha) 9m, Chanzo cha maji hili ni hitaji la kila siku na la muhimu kwenye kuchenjua Dhahabu, Makaro kuyachimba na kuyajengea angalau 2m, vitendea kazi vingine angalau 4m, Kama huna site kukodi eneo angalau 2m na mahitaji Mengineyo kama chakula, mananda ya kuishi na usafiri.

Pamoja na gharama hizo unahitaji pesa ya kudhamini wachimbaji ili walete mawe kwako hii ni kama huna nguvu ya kutosha ya kuchimba mwenyewe angalau uwe na million 20 ya ziada. Kama unataka kuchimba mwenyewe hapo ni jambo jingine maama gharama zitaruka mara dufu. Kwa ujumla ukiwa angalau na 70m kwa hali ya sasa ilivyo na ukawa site nzuri yenye maduara mengi yenye mzigo mzuri unaweza fanya kitu kwa kipindi kisipungua miezi 5.

Mwisho! Vibari ili siyo tatizo haswa kama umelenga mwalo tu, inategemea unachimba maeneo gani ambapo kuna baadhi ya maeneo wanakuhitaji usajili mwalo wako kwenye chama cha wachimbaji wa eneo husika

Angalizo! ukisikia mtu anakwambia kapoteza Million 100 kwenye uchimbaji tambua nusu ya iyo pesa ndo imeingia kazini zingine zimeliwa na matapeli
 
passion_amo1 zingatia sana huu ushauri.
 
Unakaribia kupigwa! Kwenye madini Kuna watu waliwekeza billion 5 zote "zikachumila".

Biashara ya madini na uchimbaji imetawaliwa na ushirikina, kutapeluwa na hata kupotezwa ukizingua au ukibania.

Bora fungua hardware
Ila we jamaa acha kuvunja mioyo ya wapambanaji unaushahidi?
 
hivi ukiwa na vitu gani kwenye uchimbaji madini unakuwa na uhakika wa kupata mafanikio?
Biashara ya madini ni probability labda madini ya matani au kilo ndo ya uhakika na sio gemstone au dhahabu huku Pana mengi ya utaalamu,technology na siri
 
Kwasisi wafanyabiashara zipo biashara zenye uhakika wa mafanikio...kwa comment uliyoweka inaonyesha kabisa haujawahi kufanya biashara yeyote
Hakuna biashara hio isiyo na hasara labda ya ufisadi upate mrija WA kula Kodi zetu
 
Kuna biashara yenye uhakika wa mafanikio 100%? Kama ipo bora ufanye hiyo.

Uchimbaji ni kama biashara zingine zote basics ni zile zile hakuna kitu kipya. Uwe na eneo lenye deposits ya hayo madini, vibali, vifaa, utaalam na mtaji. No more, no less.
✅👏👏👏🙏
 
Back
Top Bottom