Wataalamu wa Sheria, naombeni mnisaidie

Wataalamu wa Sheria, naombeni mnisaidie

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Ikitokea mtu kakamatwa kipindi A ambapo Sheria inasema hivi halafu pakatokea mabadiliko ya Sheria ambapo labda kwa Sheria za kipindi A angekutwa na hatia na kuhukumiwa lakini hukumu ilichelewa na kuja kutolewa kwenye kipindi cha mabadiliko ya sheria. Je, utaratibu upi utatumika kumhukumu?
 
Je, utaratibu upi utatumika kumhukumu?
Hukumu inapaswa kutolewa kwa mujibu wa Sheria inayotumika wakati wa kutoa hukumu hiyo
=
hukumu ilichelewa na kuja kutolewa kwenye kipindi Cha mabadiliko ya sheria.
Pia hukumu itategemea aina ya mabadiliko yaliyofanyika kwenye sheria.

Mambo mawili yanayoweza kutokea kwenye mbadiliko ya sheria:
  1. Sheria mpya inayobadilisha kifungu cha Sheria ya zamani: Katika hali hiyo, kama kifungu cha Sheria ya zamani ambacho mtuhumiwa anashitakiwa nacho kimebadilishwa au kufutwa kabisa na Sheria mpya, basi mtuhumiwa hawezi kuhukumiwa wala kutiwa hatiani kwa kifungu hicho cha Sheria ya zamani. Hii ni kwa sababu Sheria mpya inakuwa na nguvu ya kuondoa Sheria ya zamani.

  2. Sheria mpya isiyoathiri kifungu cha Sheria ya zamani: Katika hali hiyo, kama Sheria mpya haikuathiri kifungu cha Sheria ya zamani ambacho mtuhumiwa anashitakiwa nacho, basi utaratibu wa kumhukumu utategemea na kama mtuhumiwa alifanya kosa kipindi cha Sheria ya zamani au baada ya Sheria ya zamani kuondolewa na Sheria mpya kuanza kutumika.

    2.1 Kama mtuhumiwa alifanya kosa kipindi cha Sheria ya zamani, basi atahukumiwa kwa mujibu wa Sheria iliyokuwepo wakati wa kosa hilo.

    2.2 Kama alifanya kosa baada ya Sheria ya zamani kuondolewa na Sheria mpya kuanza kutumika, basi atahukumiwa kwa mujibu wa Sheria mpya.
 
Sheria mpya ndio inatumika siku zote, hata leo hii bangi ikihalalishwa wale wote waliokamatwa kwa makosa ya bangi wataachiwa.
Ikitokea mtu kakamatwa kipindi A ambapo Sheria inasema hivi halafu pakatokea mabadiliko ya Sheria ambapo labda kwa Sheria za kipindi A angekutwa na hatia na kuhukumiwa lakini hukumu ilichelewa na kuja kutolewa kwenye kipindi Cha mabadiliko ya sheria. Je, utaratibu upi utatumika kumhukumu?
 
Inategemea. Soma hii excerpt from a certain judgement!

The best cited paragraph on the subject is found in the precedent of Municipal of Mombasa v. Nyali Limited (supra) and for purposes of appreciation of the present appeal, I will quote:

Whether or not legislation operates retrospectively depends on the intention of enacting body as manifested by legislation.
In seeking to ascertain the intention behind the legislation the courts are guided by certain rules of construction.

1. One of these rules is that, if the legislation affects substantive rights, it will not be construed to have retrospective operation unless a dear information to that effect is manifested;

2. whereas if it affects procedure only, prima facie it operates retrospectively unless there is good reason to the contrary.

wengine watakuja wakusaidie zaidi
 
Ikitokea mtu kakamatwa kipindi A ambapo Sheria inasema hivi halafu pakatokea mabadiliko ya Sheria ambapo labda kwa Sheria za kipindi A angekutwa na hatia na kuhukumiwa lakini hukumu ilichelewa na kuja kutolewa kwenye kipindi cha mabadiliko ya sheria. Je, utaratibu upi utatumika kumhukumu?
Katika hali ya kawaida, sheria haitumiki kurudi nyuma (retrospectively, hivyo atapewa adhabu kwa ile sheria iliyokuwepo wakati kosa linatendeka.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Sheria mpya ndio inatumika siku zote, hata leo hii bangi ikihalalishwa wale wote waliokamatwa kwa makosa ya bangi wataachiwa.
Una potosha...sio vyema kujibu kila kitu kwa kutumia ufahamu wako, pasipo elimu husika.
 
Back
Top Bottom