Hili ni tatizo kwa watu wengi sana kwenye nyumba zao. Fuatilia hapa chini..
Waya wowote, huwa una uwezo wa kubeba CURRENT kiasi fulani kwa kiwango cha juu. tazama jedwali hapa chini
View attachment 2698411
Extension cable nyingi ni za 1.5 au 2.5 square millimeter na chache sana ni za 4 square millimeter (Cross section area) na ni home made
Wengi wetu, tuna extension cable za 1.5 square millimeter tunazonunua dukani. Wakati tunachomeka vifaa kwenye extension cable, huwa hatuangalii tunachomeka kifaa chenye kuhitaji current kiasi gani, na hatuangalii tunachomeka vifaa vingapi kwenye extension cable moja.
Hebu fikiria, umechomeka pasi ya umeme yenye power ya 2kW, kwa 220V, hapo unazungumzia 9A. Halafu extension cable hiyo hiyo iwe na TV, Radio, etc HALAFU UKUTE NI 0.9 sqr mm huku imeandikwa 1.5 sqr mm. Na wengine mnachomeka pasi mbili kwa wakati mmoja kwenye extension cable moja.!!!
Kwa kawadia, waya wowote una resistance (ukinzani) ambayo kwa kupitisha current kwenye waya huo, joto hutokea. Sasa ukubwa au kiwango cha joto hutegemea kiasi gani cha current kinapita kwenye waya huo. Kiwango cha joto, kikifikia joto la kuweza kuyaunguza magamba (insulation) ya waya, moto hutokea kama ulivyooneka kwenye picha yako.
Waya zipo kwa standard kwa maana ya size. Lakini kwa bahati mbaya, watengenezaji wengi huwa hawafikii starndard hiyo. Utaandikiwa waya ni wa 1.5 sqr mm lakini kiuhalisia ni chini ya hapo.
KUZUIA HAYO, HAKIKISHA UNA SWITCHED SOCKETS ZA KUTOSHA KWENYE NYUMBA YAKO ILI KUPUNGUZA MATUMIZI YA EXTENSION CABLES NYUMBANI KWAKO.