Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Sasa hivi kinachoendelea katika ligi yetu sio kitu cha kawaida, sio tena uwezo wa kocha wala wachezaji, ndio maana unaona kocha anafukuzwa leo na kesho timu inapata matokeo kama kawaida, kocha wala sio ishu hapa bongo, ishu iko kwa wataalamu wetu wanaojua kuchomeka vijiti kwenye mageti, golini na uwanjani.
Mchezo wa Fountain Gate vs Simba ulinifikirisha sana, hasa pale washambuliaji Leonel Ateba na Mukwala walipogongana wenyewe kwa wenyewe na kushindwa kupachika wavuni goli la ushindi, mchezo wenyewe tangu awali namna magoli yalivyokuwa yanaokolewa kindumba na kipa wa Fountain yalionyesha wazi kabisa kuwa 'Kijiti' kimewekwa ili Simba asishinde.
'Kijiti' kikawekwa tena kule kwenye mechi na wajeda jana, cheza weeee lakini wapi, hangaika kule na huku hakuna goli.Kijiti kile.
Leo tena 'Kijiti" kiliwekwa pale KMC ambapo kama sio 'KIjiti" leo wajela wajela wangekula hata bao 8, 'Kijiti' kimewasaidia kupunguza mabao, na leo aliyepewa mikoba alikuwa beki wetu wa kulia ambaye alipewa man of the match.
Sasa hivi sio tena uwezo wa wachezaji, jana nilimuona Pacome akishika taulo la kipa wa JKT akitafuta Kijiti kilichomekwa wapi lakini wapi.
Kijiti kitaamua nani awe bingwa msimu huu, kama huna wataalamu wazuri wa kuchomeka vijiti sahau ubingwa.
Ni mwendo wa Kijiti tu sasa hivi.