Wataka uchunguzi ufanyike

Wataka uchunguzi ufanyike

Teleskopu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
702
Reaction score
767
Ni katika kujiuliza tu ndugu zangu.

Maseneta wa jimbo la Oregon Marekani, Kim Thatcher na Dennis Linthicum, wamewasilisha ombi la kutaka kuitishwa kwa baraza la uchunguzi (Grand Jury) ili kuchunguza kile wanachoita: “CDC’s Willful Misconduct to Hyperinflate COVID-19 Data Following Federal Law Violations.”

Yaani: CDC kuvunja miiko ya kazi kwa makusudi na kutia chumvi sana data za uviko-19 kufuatia ukiukaji wa Sheria za Nchi.”

[“Kutia chumvi sana data” yamkini wanamaanisha kuwa kama watu walikufa 10, basi CDC wangesema wamekufa 100 au 200, nk]

Ombi rasmi la uchunguzi huo liliwasilishwa kwa niaba ya watu 62,200 waliolisaini – saini ambazo zilikusanywa na Stand for Health Freedom.

Ombi hili linasema:
The official letter included eight exhibits and 20 references for evidentiary materials showing a clear need to formally investigate the agencies for willful misconduct.

Yaani:
Barua rasmi ilijumuisha vizibiti 8 na rejea 20 za mambo yanayotoa ushahidi vikionyesha uhitaji ulio wazi wa kufanyika uchunguzi rasmi wa vyombo hivyo (yaani CDC na FDA) kwa ukiukaji wa makusudi wa miiko ya kazi.

MASWALI YETU
  1. Wenzetu wanaotuletea mambo haya wana mashaka, wanakataa, wanadai uchunguzi.
  2. Sisi tunaoletewa tunadai ni salama na tunasema “tumechunguza” na kujiridhisha.
  3. Kwa nini wenzetu wanakataa iwapo waliochanjwa tayari ni mamilioni?
  4. Je, hawajaona mazuri kwenye jambo hili hadi waanze kulalamika?
  5. Mbona hawagomei chanjo ya surua na chanjo zingine?
Je, hatudhani kuwa tunachezea na kuitupa mavumbini fursa nzuri ya kujifunza kwa makosa ya wengine na kuepuka hatari?

CHANZO: Oregon Senators File Formal Grand Jury Petition Calling for Investigation into CDC’s Willful Misconduct to Hyperinflate COVID-19 Data Following Federal Law Violations - geopolitic

EE MUNGU WA MBINGUNI TUSAIDIE.
 
Back
Top Bottom