Wasi wasi wangu ni vijana wetu wanaosoma shule za kata, hazikizi mahitaji ya watoto wetu wanao soma shule hizi. Kwa maelezo ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Kawambwa, kwamba wale watakaofeli F2 chini ya wastani 30% wataruhusiwa kurudia mara moja, na endapo atashindwa mara ya pili, itabidi aendelee na mfumo husiyo kuwa rasmi. Je kama mwanafunzi anafike kidato cha nne hajui kusoma na kuandika, atawezaje kufaulu kidato cha pili? Mimi nadhani serikali kwanza ingejipanga pamoja na walimu hasa kwa shule zetu hizi zisizo kuwa na walimu wa kutosha, na baada yakutatua tatizo la walimu, ndipo tuendelee na utaratibu huu, la sivyo watakuwa wanawaonea vijana wetu.