Watakaofeli kidato cha pili - kuruhusiwa kurudia mara moja tu

Watakaofeli kidato cha pili - kuruhusiwa kurudia mara moja tu

Oscardious

Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
24
Reaction score
0
Mtihani wa kidato cha pili unaanza leo nchini kote. Serikali imerudisha utaratibu ulikuwepo hapo mwanzo wa mchujo. Waziri wa elimu amesema.
 
Waziri wa elimu amesema..................mi sijui!!
 
Wasi wasi wangu ni vijana wetu wanaosoma shule za kata, hazikizi mahitaji ya watoto wetu wanao soma shule hizi. Kwa maelezo ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Kawambwa, kwamba wale watakaofeli F2 chini ya wastani 30% wataruhusiwa kurudia mara moja, na endapo atashindwa mara ya pili, itabidi aendelee na mfumo husiyo kuwa rasmi. Je kama mwanafunzi anafike kidato cha nne hajui kusoma na kuandika, atawezaje kufaulu kidato cha pili? Mimi nadhani serikali kwanza ingejipanga pamoja na walimu hasa kwa shule zetu hizi zisizo kuwa na walimu wa kutosha, na baada yakutatua tatizo la walimu, ndipo tuendelee na utaratibu huu, la sivyo watakuwa wanawaonea vijana wetu.
 
maksi 30?, huo si mchujo ila ofa!

hata mi nashangaa. Kuna veta jamani, watakaoshindwa kunawafaa. Sio kila mtu ana kipaji cha kukariri maandishi. Kuna dogo mi namfahamu yuko wilaya ya makete alifeli form four sasa hivi ametengeneza umeme kwa utaalamu wake na kijiji cha ipelele wanautumia. Nimepewa taarifa kwamba kijiji cha ivalalila nao wamemuita awatengenezee umee baada ya ule wa tanesco ulio umbali wa km moja kushindwa kuwafikia. Mtu kama huyu angewezeshwa mambo ya ufundi toka enzi hizo angekuwa mbali sana. Wengine wanapata mara tatu za hizo kwa nini tuwalazimishe wanaoshindwa? 30??
 
Ole wako waziri wa elimu .Shukuru Kawambwa !mnafiki,kwa kuwa hukuwahi kusoma elimu ya kuchagua jibu Sahihi katika somo la hesabu maisha yako yote.
OLE WAKO FILIPO MULUGO kwa kuwa umepelekea wadogo zetu mwaka huu kwa elimu ya msingi kufamya mtihani wa kusiliba jibu.
OLE WENU CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUKIWEKA KIZAZI CHA WATANZANIA NJIA PANDA.huku watoto wenu wakisoma shule ng'ambo.huku mkitupa sera mbovu kwa elimu.
OLE WENU WABUNGE KWA KUNYAMAZA KIMYA bila ya kuwakanya Shukuru kawambwa na Mulugo.
OLE WETU WATANZANIA.kwa kuwa elimu yetu ilianza kupigwa dana dana na aliyekuwa waziri wa elimu MUNGAI kwa kuanza na kufuta ekimu ya ufundi.shule niliyosoma mimi Moshi technical imeyumba kitaaluma mpaka leo baada ya walimu kukosa moyo wa kufundisha masomo ya ufundi.yaliyokuwa mkombozi wa watoto wa wanyonge na kupigia debe vyuo vya VETA.ambapo Wewe Mungai ulinufaika ama moja kwa moja ama ulipata maslahi kwa walioanzisha VETA.funga kazi ni huyu KAWAMBWA NA MULUGO.Mungu bariki TANZANIA.
 
Ni hoja nzito iliyotolewa kwa lugha inayovuta hisia. Lugha ya masikitiko lakini natumai sio lugha ya kukata tamaa. Ni onyo kati ya maonyo kama Kiswahili changu kiko sahii ambayo waandishi mashuhuri wamekuwa wakituhasa na kuiambia serikali isiyosikia. Jenerali Ulimwengu ni miongoni mwa waandishi ambaye ametahadhalisha mara nyingi jinsi ambavyo Tanzania tunacehzea mambo muhimu kama elimu halafu tukitegemea kurndelea. Kama viongozi wetu wanafikiri kwa kuwapeleka watoto wao nje na kutuachia elimu ya majaribio, ya fastafasta ndio wao watafahidi wanajidanganya maana hata wakirudi wao nchini na kushika vyeo vya juu hatafaulu maana watakutana na watu ambao hawawezi kuongea lugha moja. Watajua mengi lakini watafanya kazi katikati vhiyo na wao hawatafika mbali katika vyeo watakavyoshika. Ni bora tuanze kushughulikia hali hii toka sasa tusisubiri mabaya yatokee. Tulinyamaza na kujengewa shule za kata zisizokuwa na walimu na vuitendea kazi. Si mbali sana matunda yake tutaanza kuyavuna. Sasa hili na kuzungusha jibu la kuchagua ni kitanzi. Ni hatari lakini hata kabla hali haijaanza shule za msingi kuna vyuo vikuu hapa Tanzania katika ngazi ya Masters wanawaletea wanafunzi mitihani ya aina hiyo na kuwawekea mistari ili wajaze majibu. Wanalazimisha majibu yatokane na notices walizotoa wao lecturers. Wakiulizwa wansema namna ya kujibu ni American au Japanese style. Elimu yetu inachezewa maana wanafunzi wananyimwa fursa za kujisomea hivi wakawa na wigo mpana wa kufanya analysis. Sasa tattizo ni kubwa maana lingeanza kupigwa vita na wasomi lakini ukikutana na mtu mwenye shahda ya uzamivu anashabikia mambo kama hayo uone kuwa ni hatari
 
Waziri wa Elimu shukuru Kawambwa ametangaza leo kwamba, mwanafunzi yeyote atakayeshindwa mtihani wa kidato cha pili mara mbili atafukuzwa shule moja kwa moja.

Swali langu, wakishafukuzwa shule hawa wanafunzi, wataenda wapi hawa watoto katika mazingira ya sasa.... Ukahaba, wizi. Nani atawahajiri watoto waliofeli Form II ????
 
Swali langu, wakishafukuzwa shule hawa wanafunzi, wataenda wapi hawa watoto katika mazingira ya sasa.... Ukahaba, wizi. Nani atawahajiri watoto waliofeli Form II ????

kwani hata sisi tulio soma nani anatuajiri? Si tupo tu kitaa tukihaha huku na huko! We acha tu bwana najuta kuzaliwa bongo
 
Back
Top Bottom