Watakaopata daraja la 4 na sifuri elimu ya sekondari watashtakiwa kwa uhujumu uchumi

Afisa Elimu wa Mkoa Kilimanjaro, Paulina Mkwama amesema watakaopata chini ya Division 3 wajiandae kushtakiwa kwa uhujumi Uchumi.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Umbwe walipokuwa katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Gerald Mweri.

Amesisitiza kuwa Serikali inagharamia kwa kulipa mishahara walimu na watumishi wa elimu halafu wakapata division 4 au sifuri, haikubaliki na wajiandae kushtakiwa kwa uhujumu uchumi.

Shule ya Sekondari ilikuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kutokana na uchakavu wa mabweni ambapo sasa imekarabatiwa hivyo itaweza kuchukua wanafunzi 700.

Uhujumu uchumi kwani wamewalazimisha kuwalipia ada? Si mmetaka wenyewe?
 
Sijui baadhi ya viongozi wa awamu hii ya tano wakoje?

It's like huwa hawapimi maneno yao kabla hayajawatoka kinywani.

Huyu Afisa Elimu Mkoa ameshindwa kujifunza kwa waliomtangulia namna ya kupandisha ufaulu??

Au yeye ndiyo Mtu wa Kwanza kushika hiyo nafasi ya afisa Elimu??

Namshauri apitie sheria ya makosa uhujumi uchumi hapa 👇👇
 
Attachments

Sijui baadhi ya viongozi wa awamu hii ya tano wakoje?

It's like huwa hawapimi maneno yao kabla hayajawatoka kinywani.

Huyu Afisa Elimu Mkoa ameshindwa kujifunza kwa waliomtangulia namna ya kupandisha ufaulu??

Au yeye ndiyo Mtu wa Kwanza kushika hiyo nafasi ya afisa Elimu??

Namshauri apitie sheria ya makosa uhujumi uchumi hapa [emoji116][emoji116]
Hawajui cha kufanya hawana mbinu za kusaidia vijana wetu vimebaki vitisho tuu!!
 
Anatania au yupo serious?

Kama yupo serious basi ilibidi yeye awe wa kwanza kushtakiwa kwa uhujumu uchumi.
 
Hawajui cha kufanya hawana mbinu za kusaidia vijana wetu vimebaki vitisho tuu!!
Ujinga tupu

Wameshindwa kutoa angalau zawadi kuongeza Morale kwa walimu pamoja na wanafunzi wanaofanya vizuri wanaishia kuwatisha Wanafunzi
 
Hivi kufeli mtihani ni kosa la jinai ?
Au ni la madai ?
Au ni kosa la kinidhamu ?

Mbona mimi naona kama sio kosa.
Nikosa TU...HALIPO kwenye hayo tajwa lakini nikosa...

Nikosa kukosa Akili darasani...nikosa kuwanazo na ukakosa Ajira... Nikosa kufeli darasa lasaba na usiwe mfanyabiashara mkubwaa...

Wote tajwa washtakiwe tu..

Nikosa kuwa mkurya alafu hujapiga mtu panga la kichwa Billie ... Ushtakiwe
 
Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama amesema wanafunzi watakaopata daraja la nne na sifuri (Division 4 & 0) katika shule ya sekondari ya Wavulana ya Umbwe wajiandaw kushitakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi. Amesema kwamba haiwezekani mwanafunzi usomeshwe na serikali kwa kutumia hela za serikali halafu utegemee kupata Division 4 au 0.
Huyu naye hajielewi.
 
Akija mgeni toka Burundi Leo halafu afungulie tiivii akute habari ya kwanza Ni hii ya Mkwama.
Habari ya pili Ni waziri wa elimu akiwafokea wachina kwa kiingereza, habari ya tatu Ni waziri wa nishati akisema ambao watakua hawajafungiwa umeme watapelekwa polisi, habari ya nne Ni mh. Chala Mila akiongea kuhusu kumbusu mtu ambae humjui, habari ya tano Ni bungeni ambapo mbunge mmoja anaongelea kuhusu large sex payers na Ile ya building and Finance na ya mwisho Ni mzee Halima akiapishwa.
Hahahhahahaaa......naipenda Tz akya nan......!!
 
Nauliza tu wakisoma wote mtawapeleka wapi waliopo tu wanawashinda

Hahaha hii ndo tz tutaona mengi 🏃
 
Afisa Elimu wa Mkoa Kilimanjaro, Paulina Mkwama amesema watakaopata chini ya Division 3 wajiandae kushtakiwa kwa uhujumi Uchumi.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Umbwe walipokuwa katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Gerald Mweri.

Amesisitiza kuwa Serikali inagharamia kwa kulipa mishahara walimu na watumishi wa elimu halafu wakapata division 4 au sifuri, haikubaliki na wajiandae kushtakiwa kwa uhujumu uchumi.

Shule ya Sekondari ilikuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kutokana na uchakavu wa mabweni ambapo sasa imekarabatiwa hivyo itaweza kuchukua wanafunzi 700.

Huyo nae kilaza kama kabudi
 
Li nchi limeshakuwa la kipumbafu
 
Back
Top Bottom