Watakatifu ni wazungu waliokufa zamani. Waafrika waliokufa zamani eti ni mizimu

Watakatifu ni wazungu waliokufa zamani. Waafrika waliokufa zamani eti ni mizimu

Wapo Watakatifu Waafrika wengi pia wakiwemo mashahidi wafia dini wa Uganda kina Kalori Lwanga na wenzake.Shida kwa Africa Ni upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati.

Hata JPM kwa kauli zake na msimamo wake juu hatua za kukabili uviko 19 na kujitoa kwake, aliokoa maisha ya wengi kwa Imani thabiti kwa Mungu.

Kigezo hicho Pekee mbali ya madhaifu yake mengine anaweza kutangazwa Mtakatifu.


theguardian.com/world/2023/may/08/iran-hangs-two-men-for blasphemy-as-executions-increase-amid-unrest
 
Sasa mkuu kwa mashida tunayopitia duniani sisi waafrika ukija kufa et bado unatakiwa uje Tena utatue shida za ukoo! Unafikiri tutaitwaje sasa..?

Mfano wewe tu ulikujaga na ID ukajiita gilesi watu wakakushitukia wakakuumbua!

Haya tuje tukuite mtakatifu kweli! We ni mzimu tu..🤣🤣
kesi ya gilesi na taco la kutetemeka😅😅😅
 
Ni upumbavu wa hali ya juu wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kuitwa mizimu halafu wale wazungu kuitwa watakatifu, nakereka sana.

Utasikia mtakatifu Yohana utuombee. Halafu sisi tukiwaambia wazee wetu watuombee mnasema tunaabudu mizimu.

Halafu sipendi kabisa mnavyosema sisi ni wapagani. Sisi sio wapagani, ndio maana tunatambua uwepo wa Mungu Mkuu tuliye mwita kwa majina mbalimbali mfano Mulungu, Nguluvi nk.

Tunaomba mheshimu imani yetu. Makafiri na mapagani ni nyie mnaoabudu dini za magabachori
Kwani neno mizimu lina ubaya gani. Acha wao waitwe watakatifu sisi tutawaita mizimu kila mtu ashike lake. Hata majina wao wana yao ya akina John sisi tu yetu ya akina mwakingwe na hatulalamiki.
 
Hongera Mkuu kwa andiko lako! Ila sio kweli kwamba watakatifu wote ni wazungu, hawa nj baadhi ya watakatifu wasio wazungu:
Mashaidi wa Uganda, hapo kuna:
Mtakatifu Charles Lwanga (Karoli Lwanga)
Mtakatifu Matthias Muluumba
Mtakatifu Andrew Kaggwa
Mtakatifu Athanasius Bazzekuketta
Mtakatifu Gonzaga Goonza
Mtakatifu Noe Mawaggali
Mtakatifu Luke Baanabakiintu
Mtakatifu James Buzaabalyaawo
Mtakatifu Gyaviira Musoke
Mtakatifu Ambrosio Kibuuka
Mtakatifu Anatoli Kiriggwajjo
Mtakatifu Achilles Kiwanuka
Mtakatifu Kizito Omut
Mtakatifu Mbaga Tuziinde
Mtakatifu Mugagga Lubowa
Mtakatifu Joseph Mukasa
Mtakatifu Adolphus Ludigo
Mtakatifu Bruno Seruunkuuma
Mtakatifu John Mary Muzeeyi
Mtakatifu Dennis Ssebuggwaawo Wasswa
Mtakatifu Ponsiano Ngoondwe
Mtakatifu Mukasa Kiriwawaanvu

Ukiachana na hao kuna hawa:
Mtakatifu Justin de Jacobis
Mtakatifu Josephine Bakhita
Mtakatifu Daniel Comboni
Mtakatifu Jacques Berthieu
Mtakatifu José de Anchieta.

Utakatifu sio rangi wala ngozi mkuu
 
Back
Top Bottom