Watalii wa kimataifa wajiunga na sherehe ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina nchini China

Watalii wa kimataifa wajiunga na sherehe ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina nchini China

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111615984517.jpg
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina inakaribia. Siku hizi katika mitaa na vichochoro nchini China, kuna wageni wengi ambao wamekuja China kujionea na kupata uzoefu wa sikukuu hiyo muhimu sana kwa Wachina. Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina imekuwa kivutio kipya cha China kwa watalii wa kimataifa.

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Safari la China Ctrip zinaonesha kwamba, katika wiki mbili zilizopita, maagizo ya ndege za kwenda China zimeongezeka kwa asilimia 400 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki, huku watalii wa Argentina wakiongezeka mara tisa, na nchi za Ulaya zikiwemo Uholanzi, Uhispania, na Uingereza zikiongezeka kwa zaidi ya asilimia 200.

Tangu Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi ya Kichina iwekwe kwenye Orodha ya Wawakilishi wa Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu ya Umoja wa Mataifa, sikukuu hiyo imevutia na kufuatiliwa zaidi duniani. Zaidi ya hayo, katika miaka ya hivi karibuni, China imesamehe visa ya muda mfupi kwa nchi nyingi, ambapo hatua hiyo imewarahisisha watalii wa kigeni kuingia China kwa kiasi kikubwa. Takwimu zilizotolewa na Idara ya Uhamiaji wa China zinaonesha kuwa mwaka 2025, zaidi ya wageni milioni 30 waliingia China bila visa, ambalo ni ongezeko la karibu asilimia 50 kuliko mwaka 2024.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina yenye historia ya miaka elfu kadhaa inaonesha utamaduni mkubwa wa China. Sikukuu hiyo bila shaka ni moja ya vivutio vikubwa zaidi nchini China kwa watalii wa kigeni. Kutoka majengo marefu yanayoingia mawinguni jijini Shanghai hadi mandhari nzuri ya kiasili huko Guilin, watalii wa kigeni wanatembelea miji na vijiji nchini China ili kushuhudia jinsi Wachina wanavyosherehekea sikukuu yao muhimu zaidi. Taa nyekundu zinazopambwa mitaani, mlio wa fataki, na furaha kwenye uso wa watu zote hizo zinawaachia watalii wa kigeni kumbukumbu kubwa.

Nyuma ya ongezeko kubwa la watalii wa kigeni wanaokuja China kuijionea sherehe ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina, ni upendo wa watu wa nchi za nje kwa utamaduni wa China, ni pongezi zao kwa maendeleo ya China, na pia ni hamu yao ya kushuhudia maisha ya furaha ya watu wa China.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina inageuka kuwa kanivali ya kimataifa, na kukaribisha watu wa duniani kote kuwa na wakati wa furaha kubwa pamoja na Wachina.
 
Back
Top Bottom