Watalii wapatao 1000 kutoka Ukraine wadaiwa kukwama Zanzibar

Watalii wapatao 1000 kutoka Ukraine wadaiwa kukwama Zanzibar

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1646039941142.png

Serikali ya Zanzibar imesema inashirikiana kwa karibu na ubalozi wa Ukraine uliopo nchini Kenya kuangalia ni namna gani itawasafirisha watalii wa Ukraine wapatao elfu moja ambao hivi sasa wamekwama kisiwani humo baada ya kuzuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine.

Leila Mohammed Musa, ambaye ni Waziri wa Utalii wa Zanzibar ameiambia BBC kwamba, watalii hao, tayari wanaendelea kupewa huduma za kibinadamu licha ya wengine kuwa wamemaliza siku zao za kutalii.

Amesema mpango uliopo ni watalii hao kupelekwa nchi jirani ya Poland. Hata hivyo, taarifa zaidi za kufanyika kwa zoezi hilo zitatolewa pindi Balozi wa Ukraine atakapofika kutoka nchini Kenya na kufanya mazungumzo na serikali ya Zanzibar hii leo.

Baadhi ya hoteli zimelazimika aidha kupunguza viwango vyao vya bei huku nyingine zikiamua kutoa hifadhi kwa wageni hao kwa malipo madogo.

Mmoja wa watalii hao, ambaye amekuja kutembea na mama yake, ameiambia BBC kwamba, hivi sasa wana wasiwasi iwapo wataweza kurudi nyumbani kwa wakati na iwapo watamkuta bibi yao mwenye umri wa miaka 84 akiwa katika hali nzuri.

Ukraine ilifunga anga yake kwa ndege za kiraia kufuatia mashambulizi kutoka Urusi, hivyo ndege zote za abiria kulazimika kusitisha safari zake.

Zanzibar, kwa miaka mingi, imekuwa ni kivutio kwa watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani.
 
Mwenye namba ya mtoto mmoja mkali wa Ukraine anipe, ili tufanya mawasiliano ya kuja kumpa hifadhi huku kijijini nanjilinji. Hizi ni fursa ndugu zangu wazenji, acheni kuzilalia. Ingekuwa kwa wenzetu huko Nigeria, hao wageni wote wangekuwa washaisha hotelini.
 
najua wale waa... wa.... wataiondoa sasahivi.. ila msg deliver!!
 
... Hizi ni fursa ndugu zangu wazenji, acheni kuzilalia. Ingekuwa kwa wenzetu huko Nigeria, hao wageni wote wangekuwa washaisha hotelini.
Fulsa ninayoiona kwangu ni hii, yaani unapompa msaada mtalii kwenye janga kama hili sure for future days come lazima ule mema ya dunia endapo huyo mtalii ni don!.
 
Yaani wakwetu wapo mia tatu kule wamekwama wao wapo buku je na wale wetu wanapimiwa kikombe hiki hiki?
 
Kumbe tanzania kuna ubalozi wa urusi halafu ukrainia hakuna. Kumbe inapaswa tuwasapoti urusi maana ni marafiki wazuri wanaojali...
 
Raisi Mwinyi anafanya vizuri watu hawakusahau ukiwasaidia wakati wa shida

 
Fulsa ninayoiona kwangu ni hii, yaani unapompa msaada mtalii kwenye janga kama hili sure for future days come lazima ule mema ya dunia endapo huyo mtalii ni don!.
Hakika! Na ni rahisi kukufanyia mpango wa kwenda kuishi kwao kama utaridhia. Hii fursa kwa wenzetu wa nchi za magharibi kama vile Nigeria au Ghana wangeichangamkia kwa faida ya baadae, lkn ndugu zetu wavaa misuli ndio kwanza wanakimbia kwa kigezo cha kuogopa kwenda kulishwa nguruwe ulaya.
 

Watetezitv

50co35hcnamg2oc2eu75 ·

“kuna watalii kutoka Ukraine kama 900 sasa hivi wako Zanzibar na hawawezi kurudi kwao wameomba msaada ili serikali iweze kuwasaidia hawawezi kuendelea kukaa hotelini kwasababu hawana fedha lakini tumeanza mazungumzo na wale wenye hoteli pamoja na serikali kwa jinsi gani tutawasaidia hao mpaka serikali yao itakapopata uwezo wa kuleta msaada,”Dkt Hussein Mwinyi,Rais wa Zanzibar

“kuna makubaliano ambayo yameanza kuonekana ya wenye hoteli kuwapa msaada bila kuwachaji lakini na serikali kuwaangalia wale wenye hoteli kwenye upande wa kodi, tunazungumza tukipata muafaka basi tutaeleza ni kitu gani tunafanya lakini ukweli kwamba tunaona msaada kwa hawa watu ambao walioko kwao sasa wanaondoka kwahiyo huwezi kumwambia mtu rudi kule,”Dkt Hussein Mwinyi,Rais wa Zanzibar
 
Back
Top Bottom