III II II II II
New Member
- Oct 16, 2021
- 3
- 103
Naam, watanganyika ndio wazenji halisi, siyo waunguja na wapemba kama inavyoaminika kwa wengi!
Bendera ya iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Tanganyika
Nasisitiza tena, watu wa Tanzania bara ndio wazanzibari orijino.
Asili ya neno Zanzibar ni maneno mawili ya kiarabu. "Zanj" ikimaanisha 'watu weusi' na "Bar" ikimaanisha 'nchi kavu'. Neno la kiarabu 'bar' ndiyo asili ya neno la kiswahili "bara". Kwahiyo maana ya neno "Zanzibar" ni 'nchi ya watu weusi'.
Nakubali kwamba hapa visiwani wapo watu weusi lakini ukifanya utafiti vizuri utagundua wakazi wengi wa Zanzibar wana asili ya nchi za kiarabu kama Oman, Uajemi na baadhi wana asili ya India huku wachache zaidi wakiwa na asili ya Ulaya.
Majengo pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi kisiwani Unguja
Hili si jambo la kushangaza kwa sababu historia inaonesha kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana kati ya wazanzibari asilia na watu wa Asia kwa karne nyingi hapo nyuma, jambo lililochochewa zaidi na biashara haramu ya Utumwa na Utawala batili wa kisultani uliokalia visiwa hivyo kimabavu kwa zaidi ya miaka 100.
Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya kwa miaka michache niliyowahi kukaa hapa Unguja nimegundua kuwa hata wale wazanzibari wanaoonekana kufanana zaidi na watu wa bara, ukifuatilia vizuri utakuta wao pia wana damu za kiarabu au kiajemi, jambo linaloashiria uwepo wa mwingiliano wa kindugu baina yao na waasia wenyewe au machotara wa kiasia hapo zamani.
Iko wazi kwamba, hata bara kuna watu wengi wenye asili za Mashariki ya kati, Mashariki ya mbali, na wengine Ulaya lakini hilo halibatilishi ukweli kwamba watu wa aina hiyo ni wachache ukioanisha idadi yao na ya wale ambao asili zao zinatokana na jamii mbalimbali za hapa hapa barani Afrika.
Mlima Tarime mkoani Mara ukionekana kwa mbali
Kwa muktadha huo nachelea kuhitimisha kwamba Watanganyika ndio Wazanzibari halisi. Neno Zanzibar linaleta mantiki zaidi likitumika kuwaelezea watu wa bara kuliko wa hapa kisiwani.
Sisemi kwamba kuanzia leo watu wa bara tuitwe Wazanzibari lakini najaribu tu kuwafungua macho baadhi ya Waunguja na Wapemba ambao wakisikia neno Zanzibar wanajawa na hisia za kibinafsi za utaifa wa Zanzibar kiasi cha kujihisi wao ni tofauti na sisi wakati kiuhalisia neno Zanzibar linaweza kutumika kama utambulisho wa Watanganyika, na Waafrika weusi kwa ujumla.
Bendera ya Zanzibar ndani ya Muungano
Nimewahi kuishi Zanzibar kwa miaka 4 wakati bado najitafuta kabla ya kuamua kurudi nyumbani Tarime, lakini katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano mwezi huu wa nne niliona nije kujivinjari hapa kisiwani Unguja na nikutane na baadhi ya rafiki zangu baada ya kutenganishwa na umbali kwa muda mrefu kidogo sasa.
As long as I'm still alive, Tanzania must one day become one country for real. I see no point of Union if one part of the Union consider itself as a separate state!!
Bendera ya Jamhuri ya Watu wa Tanzania ikipepea kwenye mlingoti
Nimesema Jamhuri ya Watu wa Tanzania kwa makusudi kabisa.
Happy 60th Union Anniversary 🎉
Il| Il |I l| Il