Watanganyika tuache hujuma dhidi ya Zanzibar

Watanganyika tuache hujuma dhidi ya Zanzibar

Koloni letu hilo, siku walipopata nafasi ya kuwa mwanachama wa CAF nilishangaa sana lakini serikali iko makini ikacheza bonge la faulo Kudos Tanzania government
 
Tanganyika na Zanzibar wanacheza huko. Lkn kwenye screen wameandika Zanzibar na Tanzania bara. Sijui ni kwa nn wasiandike tuu Tanzania bara Vs Tanzania visiwani
Hiyo sio sawa. Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hivyo wangeandika "TANGANYIKA" versus "ZANZIBAR".
 
Hiyo sio sawa. Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hivyo wangeandika "TANGANYIKA" versus "ZANZIBAR".
Naona Neno Tanganyika halipendwi kabisa na hata na Watanganyika wenyewe.
Sielewi ni kwanini
 
Mzee unachanganya kati ya fifa na caf
😝😝😝😝 nimecheka kama mwehu, hivi unafatiliaga michezo kweli?
.
Zanzibar ilipata uanachama wa CAF na hii ingewapa wao nafasi ya kupeleka timu ya taifa kwenye mashindano yote ya CAF mfano CHAN, AFCON senior, AFCON U17,U23,AFCON wanawake n.k serikali hili ililiona mapema ikalifanyia kazi ikafutwa.
.
Imebakisha kupeleka timu shirikisho na klabu bingwa tu na hii ni leseni inayopata shirikisho la soka lolote barani Africa, Zanzibar haijawahi kuwa mwanachama wa FIFA.
Mashindano ya FIFA kuna World cup, World cup U17, U23, klabu bingwa dunia, women's word cup n.k
 
Tanganyika na Zanzibar wanacheza huko. Lakini kwenye screen wameandika Zanzibar na Tanzania bara. Sijui ni kwa nini wasiandike tuu Tanzania bara Vs Tanzania visiwani
Zanzibar ndio tatizo..kwa nini wasitumie jina lao la Tanzania visiwani? Mbona Tanzania bara hawatumii Tanganyika na hakuna tatizo lolote....

Tanganyika ilishapote na kuzikwa na Nd. Mtikila

Zanzibar inabidi ijifie au ilazimishwe kufa...hakuna namna..

Zanzibar sio Nchi.. wanalazimisha tu
 
Zanzibar walikua sahihi ila huku bara ndio ingebidi kutumia labda Kilimanjaro Stars
 
Ifikie wakati Zanzibar ipewe tu mamlaka yake kamili na hivyo kuwa nchi inayojitegemea. Huu Muungano umekaa kinafiki sana.

Yaani wana serikali yao, wimbo wao wa Taifa, bunge lao, Ikulu yao, Rais wao, Mamlaka zao za kiutendaji, nk! halafu wakati huo huo wako chini ya usimamizi wa serikali ya Tanganyika.
 
Zip features za failed State?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna uelekeo.

Watawala ilimradi wanakula basi, wakifa wanawaweka watoto wao kundi la kula basi eg Kulikuwa na umuhimu gani wa kumteua mama Salima Kikwete akajae tu mjengoni as if kuna jambo kubwa sana la msing kwa nchi au Bulembo.

Kila mtu ameacha afanye ajuaavyo ilimradi asisumbue watawala e.g Machinga.

Vyuo ni kuteuana kula tu wala si kusaidia nchi.

Mpaka sasa hakuna chocgote ambacho tumefanikiwa kama taifa, tupo tupo tu.

Hata mishahara ya watumishi tunaunga unga tu, mpaka askari tumeshindwa kuwalipa vizuri, ila kwa kuwa tunajipendekeza kwao kwa vile tunawatumia kutulindia ugali wetu basi tunasema wapande BURE daladala ingawa hakuna utaratuibu wowote official umewekwa, ni ujinga tu maana makampuni ya daladala mwaisho wa siku tunawadai kodi wakati tunataka wasafirishe baadhi ya watu bure.

Mapato sasa kila mtu anakusanya ajuavyo maana zile za TRA zikishaenda mfuko mkuu basi huku nchini hazifiki tena, Mkuu wa nchi ndio anatembea anagawa akipenda.

Sasa kila mtu akitaka kuendesha mambo yake naye anakusanya awezavyo, TRA wanakusanya, NEMC, TFDA, TRAFFIC, TARURA, TCRA, Halmashauri n.k
 
Sisi watu wa Tanganyika hatujitambui, maana ingekuwa tunajitambua tungeshadai jina la Tanganyika litumike badala ya Tanzania Bara.

Ni kwavile tu Wazanzibari wamekosa msuli wa kujinasua na ukoloni mamboleo wa Tanganyika, ila wao ni watu wanaojitambua sana kuliko sisi wa upande wa pili.
 
Back
Top Bottom