Watangazaji wa Azam TV wamekuwa wakirudia nguo

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
379
Reaction score
466
Azama Media ni moja ya kituo kikubwa ambacho kimeleta mabadiliko makubwa katika tasnia yetu ya habari hapa nchini.

Wamekuwa wabunifu katika vipindi, ubora wa picha na mpangilio mzuri wa vipindi na wingi wa channel nzuri katika king'amuzi chao, hongereni kwa hilo.

Kero ya watu wengi na wapenzi wa Azam Media ni kwamba watangazaji wengi wamekuwa wakirudiarudia nguo, yaani mpaka inakuwa kero, kuna kipindi cha Ndani ya Boksi Azam 2 na Mkanda, yaani watangazaji hawapendezi kabisa na kila nguo zinarudiwa kila wiki, hadi inaboa kwakweli.

Azam TV ni brand kubwa kwa nini kusiwe na uwekezaji katika suala hilo au watangazaji wasijiongeze kuingia mikataba na kampuni za nguo sababu hata media nyingine huwa wanafanya hivyo.

Inakera vipindi ambavyo unatamani kuona presenter akiwa smart unaona anarudia nguo ya wiki iliyopita, jamani badilikeni inaboa sana.
 
Lazima watafute watu wa mavazi wawapangilie Hawa watu
 
We unajua mtu akifanya kazi azam basi ndo ana mihela ila ukweli wanalipwa hela ya kawaida sana pale azam malipo hayaendani na brand.
 
We unajua mtu akifanya kazi azam basi ndo ana mihela ila ukweli wanalipwa hela ya kawaida sana pale azam malipo hayaendani na brand.
Dah wanatia huruma Kuna mmoja wa kipindi Cha ndani ya boksi yule msukuma anajiita Dani bandezu huwa anasuti yake haipiti wiki mbili lazima avae au Shati lake la kacha kidogo halima shebughe anajitahid
 
Mkuu umekaribia kuwa mchawi.... Yan umebakiza hatua chache sana jitahid utatoboa...
 
Mkuu umekaribia kuwa mchawi.... Yan umebakiza hatua chache sana jitahid utatoboa...
Sio uchawi mkuu Mimi ni mfatiliaji Sana wa vipindi vyao na Kiukweli ni vipindi vizuri sana tatizo pamba babaaa

Yani pamba hzohizo daily basi Bora hata waazime sikumoja moja au wawekewe uniform Kuna mmoja analifulana la picha ya ramani basi wiki haipiti kaivaa dah shida Sana
 

Acha uongo. Sio kweli kabisa.
 
Sikiliza cotent sio mavazi
 

Una lako jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…