Tetesi: Watangazaji wa kike TBC wagoma baada ya kutakiwa kuvua Hijabu zao wakati wa kutangaza

Tetesi: Watangazaji wa kike TBC wagoma baada ya kutakiwa kuvua Hijabu zao wakati wa kutangaza

Hijab ni vazi la heshima na linatakiwa livaliwe kila sku sio mwez wa ramadhan tu, wangekuwa wanavaa kila sku hao wadada wasingekutana na hayo maswahibu sasahiv coz wangekuwa wameshapata ufumbuzi mapema. Inaonekana wanavaa hvyo kwa kuogopa au kuabudu mwezi na sio stara kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwahyo mim naona hayo wanayokutana nayo ni haki yao kabisa
Kiuislamu! Mwezi wa ramadhani ni mwezi wa toba... Waislamu wengi mwezi huu hufanya ibada sana, hata wale ambao hawakuwa wenye kufanya ibada sana huongeza ibada zao! Wengine huendeleza ibada zao hata baada ya kuisha kwa mwezi, ila ramadhan, huweza kuwa ndiyo starting point yao! Hivyo hata kama utaratibu huo wameanza ramadhani si tatizo maana wanaweza kuendeleza! KUBADILIKA SIO DHAMBI, ILI MRADI IWE NI MABADILIKO CHANYA!!!
 
Islam siyo Dini ya Serikali wala ya Taifa letu. Ukiona TBC haikufai ondoka zako kwani lazima ufanye kazi TBC? Kwani wakati unaajiliwa hapo TBC uliajiliwa kwa sababu ya Dini yako au kwa sababu ya Taaluma yako? Hebu tuondoleeni ukilaza humu ndani. Taasisi za kiislam zipo nyingi sana, Kuna Radio Imani, Bakwata,Misikitini, Muslim foundation,N.k Waende huko wakaajiriwe hapo TBC hatuhitaji mavazi mengine tofauti na tuloyazoea ,Fuateni sheria za Taasisi husika hutaki sepa zako sio lazima uwepo TBC tupo wengine mtaani hatuna ajira na tunadigriiza utangazaji lakini tumekosa ajira hivyo kuondoka kwenu sisi tutapata ajira. Ondokeni haraka sana hapo ili tuje kuomba nafasi.
Mavazi uliyoyazoea wewe ni yepi? Ya kikristo? Ukristo sio dini ya serikali na hiyo TBC si ya wakristo! Hivyo, bila kujali dini unapaswa kufanya kazi TBC na huku ukiendeleza tamaduni ya dini yako bila kumkera mwingine. Ikiwa inakukera mwanamke akivaa hijabu basi hayo ni matatizo yako! Labda ikiwa leo hii utaniweka wazi kuwa TBC ni stesheni ya wakristo na hii nchi ni ya wakristo pia!!! Kingine, hijabu ni vazi la heshima kwa wanawake ndiyo maana hata masista huvaa hijabu...wasiovaa heshima F!!!
 
Walipoajiriwa TBC, Waliajiriwa kwa kigezo cha Dini yao au kwa kigezo cha Taaluma zao? Je islam ni dini ya Serikali au ya Taifa la Tanzania hadi watu wote tuitambue? Je huko Zanzibar wakristo wasiotaka kujipatiliza lundo la Manguo nao wanapewa uhuru huo? Je wamelazimishwa kufanya kazi TBC? KWANINI WASIENDE KWENYE TAASISI ZAO WAKATANGAZE IMANI YAO? Mbona wanazo taasisi nyingi tu mfano Radio koroani, Radio Imani, Muslim foundation, Bakwata, Arahamaini n.k ? Ondokeni ili sisi tusio na ajira ambao tunazihangaikia kuzipata na hatuzipati na tunadigrii zetu za utangazaji tukajipatie Ajira. Waondoke haraka sana tupate ajira sisi. Hatupo tayari kutazama miushungi yenu. Tunataka tumuone mtangazaji sura yake ili tuelewe zaidi.
Hijabu haifichi sura ndugu yangu! Sura unayotaka kuiona... Utaendelea kuiona!!! Ikiwa hauna kazi kweli na una nyodo kiasi hicho basi hutopata ajira! Hakuna bosi anayetaka mfanykazi wa kariba yako! Ukibadilika...utapata!!!
Kuvaa hijab au kujihifadhi mwanamke ni shurti, lakini hao wa hijab ya siku 30 halafu baada ya hapo wanarudi kwenye vimini na mipasua haingii akilini. Mwenyezi Mungu hajasema wanawake wajihifadhi ktk mwezi wa ramadhan tu.

Huu ni mwezi wa kuongeza bidii katika ibada lakini ucha Mungu na kujistiri ni maisha yako yote baada ya kubaleghe.
 
Kweli nimeamini Tanzania in watu ambao hawaja elimika kabisa na hawawezi kujenga hoja , jalibuni basi hata kupitia katiba muone inasemaje kuhusu dini , kama hamjui kusoma semeni

Majibu yako yanaonyesha umelimika sana! Labda nikukumbushe kitu, Taifa letu halikujengwa kwa misingi ya Dini, Ukabila nk - mambo ya Dini yawe confined Makanisani na Misikitini siyo mashuleni, kuna haja gani kutangaza Dini yako unapo kuwa shuleni kwa njia ya mavazi kwani majina hayatoshi kudhilisha Dini yako?

Mambo haya hayakuwepo siku za nyuma siku hizi yameshika kasi ya ajabu, mwanzo nilijaribu kutafuta sababu zenye mshiko nikashindwa, lakini baada ya kufanya kautafiti kidogo nikagundua hii ni njia moja wapo ya kutaka kutuma ujumbe kwa Watanzania ili tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini na hii ni mbaya sana kwa kuwa inanzia shuleni primary na sekondary, mnawajenga watoto akili gani kisaikolojia - na kwa nini Serikali haija liona hili!!

Sisemi mambo ya kubuni - nenda shule ya Primary au Sekondary wakati wa mapumziko au wanakwenda lunch au nyumbani utakuta wasichana wa Dini fulani masaa yote wapo pamoja kwa nini?? Hawachanganyikani na wenzao hata kidogo,w nisijue Darasani wanakaa mkao upi yaani kama utengano huo unaendelea au la?

Hii ni hatari sana kwa umoja wa Taifa letu - chunguzeni ninacho kisema hapa - hali sio nzuri hata kidogo - the sooner we address utengano huu unaojengeka siku hadi siku the better . Nayasema haya kwa nia nzuri tu.
 
TBC kikiwa kama chombo cha propaganda za serikari chenye jukumu la kujenga umoja watanzania kwenye nchi ambayo ratio za dini aziko mbali. Nitashangaa sana kama hili tamko lina ukweli.

For staters mkurugenzi wake ni katika teuzi chache sana alizofanya raisi ambazo the person is fully qualified and skilled for the post sidhani kama anaweza kuja na upuuzi kama huu given the sensitivity of the issue, his background on media representation, his task and the timing; it just doesn't make sense.
 
Kila sekta inamavazi yake, polisi wanamavazi yao kulingana na haiba ya kazi yao, Hivyo hiyvo na kwa Watangazaji,Mafundi magari,umeme,bomba na Wanajeshi, Magereza Mgambo n.k Je huko kote mbona hamdai kuvaa hijabu? Mfano fundi wa ngzo za umeme mbona hamdai kuvaa hijabu?
 
Hao watimuliwe kazi haraka iwekanavyo, Hawakuajiliwa kwa kigezo cha Dini yao, Waliajiliwa kwa kigezo cha Taaluma zao, Na waliahidi kutii sheria na kanuni za shirika husika, Waondoke waende wakaajiriwe kwenye taasisi zao kuwa Wasemaji wa Bakwata, Muslim foundation, Redio koroani, n.k TBC tunataka watu wasiojitambulisha Dini yao kwa mavazi.
 
Mbona na sekta zingine hamdai kuvaaa Hijabu? Mfano Jeshini, au hawa mafundi wa nguzo za umeme mbona hamdai kuvaa hijabu huko?
 
Kifupi ni hivi. KILA KAZI INA MIIKO YAKE, INAMAVAZI YAKE. usilete mavazi ya kwenu kuja kwenye vyombo vya umma.
 
Watii sheria za mwajiri wao au la waache kazi. Hatubembelezi mtu. Tupo wengi wenye Digrii za utangazaji na hatuna kazi badala yake tumebaki kuwa watangazaji wa Jamiiforums tu.
 
hijabu vaa ukiwa nyumbani kwako, Msikitini mtaani kwako, ukifika kazini badili nguo vaa uniform za taasisi husika, kama wewe ni mtangazaji vaa uniform yako, kama ni mhudumu wa bar vaa uniform yako, kama ni askari vaa uniform yako, kama ni mhudumu wa gesti vaa uniform yako, kama ni mvuvi vaa uniform yako, kama ni mkulima vaa uniform yako kulingana na mavazi ya kazi husika
 
(NIMEIKUTA SEHEMU HII MWENYE UHAKIKA ATUJULISHE ZAIDI)

TAFADHALI KWA WAISLAM NA WAPENDA HAKI TUFUATILIE HILI KUJUA UHALISIA WAKE.

Kuna taarifa kua watangazaji wa kike Waislam wa TBC TV wamegoma baada ya uongozi kuwataka kuvua hijab wanapotangaza.

Ieleweke ya kuwa wengi wao hupenda kuvaa hijab hususan katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Taarifa zinadai kesho asubuhi kuna kikao kujua hatma yao.

TBC TV ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi zinazotokana na wananchi wa Tanzania ambao Waislam ni sehemu ya walipa kodi.

Ikithibiti hivyo itaonesha ni namna gani nchi zetu zinakoelekea, asiyejisitiri anaheshimika na anaejisitiri anatakiwa kuvua sitara yake..

Kila sehemu na taratibu zake na kila kazi na maadili yake. Kodi za waislam hazishinikizi ajira na kukiuka taratibu. Na kutokuvaa hayo madudu hakumzuii muislam kupata huduma za TBC. Mbona kuna sehemu wanapoingia wanatoa hayo madudu? Kama vile Hawa ghasia alivyolazimisha kwamba watu wote wakiingia utumishi wavae hijabu, haikuwa na maana kwamba wizara ya utumishi ilikuwa inamilikiwa na waislam au iliendeshwa bila kodi za Watanzania.

Ni suala la kuongea na wala halihusiani na dini. Nini logic ya kuwavalisha watu hijab kwakuwa tu wanakwenda wizara inayoongozwa na mtu wa aina ile? Ofsi ni yake binafs? Vivyo hivo TBC, ni halalli kufungamanishwa na dini hasa ikiwa ni chombo cha srikali ambacho hakina dini? Kwa nini kusiwe na stadard za serikali ambazo zitasimamia ofisi zote za umma kwa wafanyakazi na watanzania badala y aushenzi wa kila kiktu kukioanisha na dini tena dini yenye makelele, porojo na ushetani ni moja tu duniani na ukizingatia watu wake hawana uelewa wa mambo, hawaridhiki hata wakifanywa nini na mwisho wake wanataka wakubaliwe watu wote wafe duniani wabaki peke yao?

Vyombo vya srikali havipashwi kushinikizwa kuendehswa kwa misingi ya dini yoyote. Serikali na Watanzania hawapashwi kushinikizwa kufuata li dini hasa linaloendeshswa kishetani. Jambo kubwa, serikali iwe na standards zake za Kitanzania ambazo kila mtu atatemembea humo. Masuala ya dini, kabila sijui na nini ,yabaki kwenye maisha binafsi ya mtu.

Vinginevyo, wamasai nao watataka waruhusiwe kutangaza wakiwa na Lubega, ukaria kichwani na mikuki!, mambo ambayo hata hatujui yanatokea wapi na yana maana gani. Wakiwa TBC wavae kama sheria wakitoka, wavue nguvo na wapitie mikuki yao!.
 
Sidhani kama ni kweli.
Citizen TV ya Kenya iliyo bora ukanda wa East Africa wanaachia Kina Lulu Hassan siku zote wakijimwaga
Yote kwa yote ni haki yao Kugoma kama wamelazimishwa Kukaa vichwa wazi.
Naunga mkono Maamuzi yao na Mungu awazidishie kwa kujitambua na Kutaambua Maamrisho ya Allah
Wameyatambua mwezi huu tu?
Mbona siku za nyuma hawakudai hiyo wanayoiita haki yao?
 
Hao watimuliwe kazi haraka iwekanavyo, Hawakuajiliwa kwa kigezo cha Dini yao, Waliajiliwa kwa kigezo cha Taaluma zao, Na waliahidi kutii sheria na kanuni za shirika husika, Waondoke waende wakaajiriwe kwenye taasisi zao kuwa Wasemaji wa Bakwata, Muslim foundation, Redio koroani, n.k TBC tunataka watu wasiojitambulisha Dini yao kwa mavazi.
Wewe kama nani TBC kutaka watu watimuliwe kazi? roho mbaya yako peleka Burundi huku, kwani hijab zinazuia nini mtu kufanya kazi mbona kuna viongozi wakubwa Serikalini wanavaa hijab na mambo yanaendelea kama kawaida..! au bungeni watu wanavaa kanzu na kofia, soma katiba ww ujue utaratibu wa imani ulivyo..!
 
Kama ni kweli,Jana nilimwona Asha Haji katupia hijab nyekundu.Kiukweli alikua hajapendeza kabisa, na huenda kuna watu walitoa taarifa uongozi wa TBC, kwani aliifunga ka mtu ambaye hajui inafungwaje na kuvaliwaje.

Nadhani inabidi Zuhra Yunus apewe mchongo wa kuwafundisha jinsi ya kuifunga. kwani hata tai sio kila mtu anajua kuifunga.

hapo nadhani ni sahihi, kwa hilo kuhusu uvaaji au ustadi wa kufunga, pengine mtu huonekana hajawa katika kiwango kinachohitajika kulingana na jinsi gani amevee,,,,,,,,,,,
wakifunga vizuri nadhani hakuna shida (kama walifunga vibaya lakini,,,namaanisha kufunga ushungi wao)
 
Back
Top Bottom