Watangazaji wa kizazi hiki wanakera mpaka basi. Hivi wanaokotwa wapi hawa viumbe?

Ndugu Pascal Mayalla hivi siku hizi taaluma ya utangazaji inachukuliwaje? Ni nani anayetoa leseni kwa watangazaji na huwa anaangalia kigezo gani? Nakumbuka zamani kazi ya utangazaji ilikuwa inaheshimika sana.
 
Hahahaha! Unakumbuka wale waandishi wa TBC walioripoti kuwa Trump amempongeza Magufuli? Walipewa adhabu na Dr Ayubu Ryoba (Mkurugenzi); baadaye wakayeyushayeyusha mambo yakaishia hewani. Watu wa vyumba vya habari hawako makini kama walivyokuwa makini wanahabari wa BBC, DW na redio nyingine za nje. Huwezi kuwasikia wakitangaza ujinga hata siku moja.
 
Ndugu Pascal Mayalla hivi siku hizi taaluma ya utangazaji inachukuliwaje? Ni nani anayetoa leseni kwa watangazaji na huwa anaangalia kigezo gani? Nakumbuka zamani kazi ya utangazaji ilikuwa inaheshimika sana.
Sahv ili uwe mtangazaji hakuhitaji uwe umesomea...
Media nyingi sahv kwanza habari zao ni udaku,michezo,miziki na maujingujing tu

Ova
 
Sahv ili uwe mtangazaji hakuhitaji uwe umesomea...
Media nyingi sahv kwanza habari zao ni udaku,michezo,miziki na maujingujing tu

Ova
Halafu media nyingi sasa hivi wanachezesha tu kamari. Kila media ina namba ya kucheza kamari. Wanataka kuigeuza nchi kuwa taifa la wacheza kamari (Tanbet).
 
Karibu CNN, Aljazeera, BBC,fox news,NHK Japan,Nat Geo, discovery science. Hutajuta rafiki utstsmani utoroke kazini au kwenye shughuli Yako uwahi nyumbani
 
Nakupa jtano Kwa hili.
 
Karibu CNN, Aljazeera, BBC,fox news,NHK Japan,Nat Geo, discovery science. Hutajuta rafiki utstsmani utoroke kazini au kwenye shughuli Yako uwahi nyumbani
Hawa jamaa wako anga zingine kabisa. Taarifa zao zimejitosheleza. Sisi tunawategemea akina Mwijaku na Juma Lokole kututafutia habari unategemea utapata nini zaidi ya mataputapu?
 
Nina uhakika mkuu. Nimefanya utafiti wangu na kupata conclusion. Wewe fuatilia hali ya utangazaji wa sasa ulinganishe na enzi zile za RTD na VoK utaona kuna tofauti kubwa sana.

Kama unasema siku hizi watu wanapata taarifa kwenye gadgets zao kwa haraka kuliko kwenye redio/TV kwanini watu wananunua magazeti? Ni kwa sababu magazeti yanaandikwa kiuweledi zaidi ukilinganisha na utangazaji wa TV na redio.
 
Naunga mkono hoja.. unaweza sikiliza kipindi hakuna cha maana unachopata zaidi ya majibizano tu
 
Unaweza kunipa trend ya usomaji wa magazeti wa sasa na kabla ? Apart from wale wanaonunua kucheki tender au government notices au kuwa na proof ya kitu fulani ni wangapi wanasoma ? Ni kampuni ngapi za magazeti zimekufa kifo cha kawaida (Habari Corporations and the likes na pamoja na mengine kuamia full mtandaoni and still with less audiences)

Sasa hivi watangazaji wakiwa na audiences wanahamia kwenye ma-podcast
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…