Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 4,107
- 9,671
Hahahahahaha haujui pale kuna njaa kuliko unavyodhani.Acha uongo. Kuna media inalipa vizuri kama Azam tz?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahahahaha haujui pale kuna njaa kuliko unavyodhani.Acha uongo. Kuna media inalipa vizuri kama Azam tz?
Salum mwalim alipokuwa dtv ndiyoUnakuwa na mtangazaji Mauldi Kitenge, Eddo Kumwembe hawa hawana shule ya Uandishi wa habari ni ujanja wao na kulaghai watu. Baraka Mpenja kaenda shule ila mropokaji na wala sio mtangazaji. Fuatilia goli la Dube alivyotangaza kuna maneno aliropoka kuhusu Dube. Ama fuatilia goli la Aziz Ki alilofunga dhidi ya Simba alivyoropa maneno ya kijinga. Anaropoka baada ya kutangaza maneno ya kiswahili fasaha. Pia wamiliki wa hivi vyombo hawalipi vyema wafanyakazi wao. Mfano pale Azam media pana njaa ya kufa mtu. Na media zingine nyingi tu zina malipo hafifu kwa wafanyakazi wao.
Shule hakuna pale ujanja mwingi tu. Yeye na Kitenge hakuna kitu. Mpe script ya kiingereza Kitenge akusomee ndio utajua ujinga wake.Salum mwalim alipokuwa dtv ndiyo
Alimuingizaga eddo kumwembe
Alikuwa wanamuita anachambua ligi ya uingereza,wanamdakisha 40000-50000,Edd9 akajiongeza kdg
Ndiyo hivyo
Ova
Mother Tongue...., Ingawa Kiswahili ni lugha ya Taifa lakini bado Makabali yana-affect matamshi..., Kama vile mzungu akiongea Kiswahili anachapia au mchina akiongeza kingereza n.k.Kwa matumizi ya r na l ni tatizo la watanzania wengi na linaanzia shuleni pale anayefundisha(mwalimu)naye hajui kutofautisha r na l.Lakini kupungua kwa wasikilizaji wa radio inatokana na urahisi wa kupata taarifa kupitia simu janja
EFMHuyu anatangazia media gani mkuu?
Kweli kabisa. Ndio maana comrade Mkapa alikuwa hapendi kuhojiwa na hawa vilaza.Tanzania haijawahi kuwa na waandishi wa habari bali ni makanjanja na wababaishaji,wavivu wa kufikiri na kutafiti.
Mwandishi wa habari anatakiwa awe mtafiti na mfuatiliaji wa Mambo kiujumla,ili awe anaibua na kuufahamisha umma usioyafahamu na sio umma ndiyo umfahamishe!
Kuna vituko vingi vimejiri kiasi Cha kujiuliza hawa waandishi huwa wanajipa muda wa kujiridhisha kabla ya kuandika habari ?
Nakumbuka 2003 walimuandika Ammy Ninje anacheza ligi daraja la pili Uingereza nilikuwa nikiangalia sky nacheka Sana!
Hizo ni takataka, mpaka najiskia kutapika. Hamna kitu kabisa.Kuna hivi vi redio vya Morogoro í ¾í´®í ¾í´®
We mtu kazaliwa 2010 leo anapewa kipindi amfanyie mtu interview wakati hajuwi anasema nini au kuuliza nini, unafikiri nini kitakachojiri?Habari wanaJF?
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha na maneno mengi. Kwa mujibu wa utafiti binafsi nilioufanya hivi karibuni, usikilizaji wa redio na utazamaji wa TV umepungua sana miongoni mwa wafuatiliaji wa habari. Hili halijatokea kwa bahati mbaya bali ni kwa sababu ya kupungua usahihi wa taarifa na ubora wa watangazaji. Sote ni mashahidi jinsi Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Voice of Kenya (VoK) zilivyokuwa na watangazaji nguli ambao huchoki kuwasikiliza.
Watangazaji wengi wa redio na TV zinazochipukia kama uyoga hapa nchini wanakera mno kwa utangazaji wa ovyo na unaokosa weledi. Ukisikiliza redio na kutazama TV, hasa hizi zinazoitwa Redio/TV za Kijamii, utahisi kichefuchefu na huwezi kuendelea kusikiliza kwa zaidi ya dakika 5! Wanachotangaza ni zaidi ya utumbo. Na kibaya zaidi, hawa makanjanja hawakupitia kabisa kwenye vyuo vya uandishi wa habari. Inasikitisha mtangazaji kutoongea Kiswahili fasaha unabaki unajiuliza: hivi huyu mtu alienda shule kweli au ameokotwa jalalani? Na kama alienda shule, je, huko alienda kujifunza ujinga au maarifa? (FaizaFoxy, 2015). Yaani hawa viumbe hawawezi kabisa kujieleza kwa Kiswahili na Kingereza fasaha.
Zamani haikuwa rahisi mtu yeyote kujipenyeza kwenye utangazaji ikiwa hajui Kiswahili na Kiingereza fasaha. Na si hilo tu, mtangazaji anatakiwa kuwa na uhakika wa jambo analolitangaza. Juzi nilipata hasira sana niliposikia mtangazaji wa mpira akiutangazia umma kuwa mmiliki wa sasa wa Klabu ya Chelsea ni Roman Abramovich. Wanajiropokea tu ilmradi tonge liingie kinywani.
Utakuta mtu ana lafudhi mbovu na uelewa mdogo kama mbegu ya hardali lakini bado anang’ang’ania kuwa mtangazaji. Ni aibu kubwa. Yaani pale inapotaikiwa kuweka “r”, yeye anapachika “l”, kwa mfano mpira anatamka mpila. Ni aibu iliyoje! Na pia ni wazuri sana kwenye upotoshaji kwa mfano neno wimbo, hutamka nyimbo……..mfano: Leo nawachezea nyimbo moja ya Diamond inayoitwa Kantangaze. Ovyo kabisa!
Kwa ujumla, nchi hii ina watangazaji wenye uelewa finyu na upeo mdogo wa utangazaji. Natoa wito kwa serikali na vyombo vinavyohusika kudhibiti maudhui ya vyombo vya habari kufanya kazi yao kikamilifu ili kuzuia upotoshaji huu unaofanywa na baadhi ya watangazi makanjanja. Aidha, kiwango cha elimu na weledi wa mtu anayefaa kuwa mtangazaji kipitiwe upya. Watangazaji wasiokidhi vigezo wachujwe na kutupwa nje ya ulingo wa utangazaji. Tumechoshwa na upotoshaji.
View attachment 2628193