Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Hapana mzee uli catch vibaya kusudio languNadhani mngejua kutofautisha kwenye ukemeaji wenu kati ya maudhui na mtindo wa ufikishaji wa sanaa.
Mnapokemea maudhui kama ushoga, ngono,ulevi,umbea, uongo, uzembe katika uwasilishwaji wa sanaa kama habari, muziki, nk. Hapo ni sawa.
Lakini sasa mnapoenda mbali/kuchanganya na kuanza kukemea mtindo wa sanaa inavyowasilishwa kama matumizi ya Lugha, mandhari, mahadhi, nk. Hapo mnakosea.
Mtindo huwa unabadilika kuendana na muda.
Mfano kwenye lugha hapo, mngetakiwa kutambua sifa ya Lugha mojawapo ni kukua, lugha sio gereza kwamba lazima ujifunge kwenye kanuni na sheria za kisarufi, misamiati nk. Zilizowekwa na wataalamu kule maofisini. Kumbuka sanaa ni kioo cha jamii. Sasa kama jamii inaongea "kwendaga" basi haina budi sanaa iakisi lugha inayotumiwa na jamii.
Hata kiingereza cha leo hakikuwa hivyo miaka 500 iliyopita. Wangeng'ang'ania na wao kisibadilike ingekuwaje?
Hata lugha za matusi pia ni mojawapo wa mtindo wa ufikishwaji wa sanaa. Haya matusi yana maana na yangekuwa mabaya sana basi jamii isingeyatunga na kuyaweka kwenye kamusi.
Mfano mwingine kwenye mziki, kuna watu wanalalamika mtindo wa kisasa wa mziki haufai, unakuta mtu kama Scars anapinga mziki wa leo kwasababu mabiti ni ya Trap, yeye anataka mabiti yaleyale ya bum bap ya miaka ya 90 mpaka leo watu waimbie.
Au unakuta mzee analalamika kuwa sikuizi mnaiga wanaijeria hamna uhalisi wa kitanzania. Well, No shit Sherlock..Have you ever heard the term 'globalization'?
Katika mziki kwanza huwa nafurahishwa na mambo makuu mawili ambayo ni ubunifu na content. Beat kwangu sio kipaumbele thats why hata kwenye ngoma za Joyner Lucas nilizozikubali zilizingatia contents.
Wakina Young Lunya wanapita kwenye trap beats lakini ukiangalia katika jicho la kisanaa utaona kuna makosa mengi ukiachana na contents lakini pia hata vina utaona havipo au ni vile vya magumashi
Vina vya magumashi mfano wake ni kama ile Dear God ya Kalla Jeremiah, mle hamna vina ila kwa wasiojua mziki hawawezi kuelewa. Na ndio maana nilipenda kuona hawa wagawaji tuzo wawe ni watu wanaojua mziki na sio kutoa tuzo kwaababu ya trend.
Kama wanataka kutuweka kwenye mfumo huo basi wazitafutie kipengele chao ili tuwe tunawaelewa kuliko kusema wimbo bora wakati lyrically ni zero
Ubunifu bongo umepungua au umeisha kabisa, hususani kwenye Bongo Fleva
Mfano leo hii katika kizazi cha Bongo Fleva tunao wasanii wakubwa kina Diamond nk. Hawa wasanii to be honestly they lack some creativity wameanza kufanya remake kwenye nyimbo za zamani
Na hata wakifanya nyimbo mpya walizotunga wao bado utaona wana pwaya kwenye content though wanabebwa na fame plus fan base waliyo nayo na ndio maana hata wakitoa nyimbo ya dakika 3 afu humo wawe wanajikoholesha tu bado ita trend tu.
Sasa hiyo inatengeneza mwendelezo mbovu kwa hawa chipukizi ambao wanataka kufikia malengo makubwa kupitia mziki.
Kwasababu watakuwa wanajenga dhana kichwani kuwa ili uweze kufikia level za juu za kimafanikio basi unapaswa kuimba style kama ile ile wanayoimba hawa wakubwa.