Mpetde
JF-Expert Member
- Sep 5, 2022
- 3,955
- 6,546
Hili suala Jana BAKITA walikua wanalizungumzia kwenye kipindi cha Radio, wakagusia baadhi ya maneno ambayo yanatumika vibaya na waandishi wa habari,Yaani pale inapotaikiwa kuweka kitamshi cha “r”, yeye anatamka “l”, kwa mfano mpira anatamka mpila. Ni aibu iliyoje! Na pia ni wazuri sana kwenye upotoshaji kwa mfano neno wimbo, hutamka nyimbo……..mfano: Leo nawachezea nyimbo moja ya Diamond inayoitwa Kantangaze. Ovyo kabisa!
Mfano neno :
Taradadi na Kwenda Matiti
Hayo maneno yanatumika vibaya
Taradadi ni neno la kiarabu linalomaanisha kua na wasiwasi juu ya Jambo fulani
Kwenda matiti ni neno la kibantu lenye maanaa ya kuishia/kwisha
Utakuta mtangazaji anatangaza anasema :
Muda ume taradadi
Badala ya kusema
Muda umeenda matiti
Vijana wengi kwenye tasnia ya Habari hususani hawa chipukizi hawana Kamusi ya Kiswahili Sanifu hilo nalo ni tatizo na hawakisomi Kiswahili wakakijua vizuri kabla hawajaingia kwenye uandishi wa habari mwisho wa siku wanatulisha madudu,