tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
- Thread starter
- #61
Cool down kijana; kumbuka hakuna kijiji kisichokuwa na wazee. Heshaima kwa wazee ni kitu bora. Hatuwezi kuona jamii inakengeuka na kuharibika tukakaa kimya. Kwa mfano, zamani hakukuwa na vitendo vya ushoga na usagaji lakini sasa hivi haya mambo yanafanyika hadharani. Tukiuliza kwanini haya mambo yanakuwa hivi mnasema wazee hatuendi na wakati. Hili sawa?Both are correct.
Ni sawa na kwenye mziki mnavyolalamikaga mziki wa sikuizi this and that.
Free advice for you;
Fanyeni kuwa mnasikiliza miziki yenu ya zamani tu muache kusikiliza ya sasaivi.
Kwenye news, angalieni zile recorded za miaka 20 iliyopita youtube.
Au muende hospitali kutibiwa kwasababu Nostalgia is one hell of a disease.
Because frankly speaking, hata mlalamikeje hamuwezi kubadilisha kitu.
Law of demand and supply, ukiona kitu kipo supplied kwa wingi basi ujue demand ndio inataka hiko kitu.
And it's a free market.
Maybe anzisheni stesheni yenu ya wazee afu muone how that'll go.
Muda ni ukuta, Huwezi kupambana nao.
Tatizo wazee tukikemea upumbavu huu mnaona tunawaingilia mambo yenu. Kumbuka ujinga unaotangazwa na watangazaji hawa unaathiri jamii nzima; mwisho wa siku hata mtoto wako au ndugu yako ataiga mambo ya kishoga halafu utaanza kumtafuta mchawi wakati mchawi ni wewe mwenyewe unayeshabikia ukengeufu.
Tukirejea kwenye muziki ndio mnaimba upumbavu kabisa. Wanamuziki wa zamani waliimba nyimbo za mapenzi ambazo baba unaweza kusikiliza na familia yako bila wasiwasi. Siku hizi vijana wanaimba nyimbo za NGONO ambazo zikiimbwa inabidi baba na mama waondoke kwa kuwa zimejaa matusi makubwa. Hata video za muziki zinazotolewa na vijana wa siku hizi hazina maadili hata kidogo......watu wanacheza wakiwa uchi eti mnatuambia huu ndio usasa! Mmerogwa nyie sio bure.
Huwa napata taabu sana wakati ninaposafiri kwenye basi la abiria hizi nyimbo na video zinachezwa tangu mwanzo hadi mwisho wa safari. Mtu huwezi hata kusafiri na mkweo au watoto wako kwenye basi moja kwa kuwa video na nyimbo zinazoimbwa mle zimejaa matusi yenye mwelekeo wa ngono. Inasikitisha sana.
Leo nimesikitika kuna wanaume wawili wanatangaza kule Wasafi FM kwenye kipindi cha mipasho wanaongea mambo ya kimbeya kama wanawake mashangingi. Nadhani hawa wanapaswa kupimwa tuone kama kweli ni wanaume au la. Mwanaume mzima utaongeaje mambo ya umbeya na mipasho kama mwanamke? So sad!