Watangazaji wa mpira makanjanja

Watangazaji wa mpira makanjanja

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ni pale mtangazaji wa mpira redioni anapoacha kuutangaza mpira unavyochezwa uwanjani badala yake anatangaza mpira wa upande mmoja anaoushabikia (timu yake) na kuwanyima ukweli wasikilizaji wake juu ya kile kinachoendelea uwanjani kwa wachezaji na timu zote uwanjani. Na kwa bahati mbaya anafanya hivyo kwenye redio ya umma inayoendeshwa kwa kodi za mashabiki wa timu zote nchini.

Hizi ni dalili tosha kuwa tasnia ya habari pia ina wafanyakazi ambao hawajaiva vizuri wasioweza kujiongeza. Kama wewe una mahaba yaliyopitiliza kwa timu yako nenda kafanyekazi kwenye chombo cha habari cha timu yako, vinginesho anzisha chombo chako cha habari ujimwage huko ili wananchi wapenda mpira wa miguu wawe na hiari ya kukusikiliza huko au la.
 
Haaaa haaaa unajua kuitangaza Sumba rahà sana,wasameheni watangazaji hii ni tokana na radha ya kina Ndemla. Juzi mlisema Azam leo mmegeukia Bwigane
 
Kuna shaffih Dauda yaani hafai kabisa, siku simba ikifungwa anakuwepo studio kwa kuisemea mabaya, siku ikishinda aonekani au akiwepo hafanyi uchambuzi! Leo simba kashinda ametoa tu matokeo akaamia sakata la nyoso!
 
Ila mbona Shafii ni Simba damu?
 
Kuna shaffih Dauda yaani hafai kabisa, siku simba ikifungwa anakuwepo studio kwa kuisemea mabaya, siku ikishinda aonekani au akiwepo hafanyi uchambuzi! Leo simba kashinda ametoa tu matokeo akaamia sakata la nyoso!
Wanashindwa kutenganisha huduma kwa jamii na mahaba yake binafsi akiwa kazini, afadhali kidogo Shafii anafanyia chombo binafsi kisichoendeshwa na kodi zetu kuliko akina Enock wanaofanyakazi TBC taifa.

Yule mzikilizaji ambae yuko Nanjilinji anataka kujua timu yake inachezaje kule uwanjani kwa kupitia matangazo ya redio yake lakini anakwamishwa na mtangazaji kanjanja mwenye mahaba ya Yanga, Simba au Azamu ambae muda wote anatangaza kwa nguvu na mahaba mpira unapoguswa na mchezaji wa timu yake au unapoelekea goli la timu pinzani. Huu ni upuuu--zi kama upuuzi mwingine kwa mtangazaji wa mpira wa miguu, hasa yule anaetumia TBC ya watu wote.
 
Juma Nkamia hakuwaga na mambo hayo enzi zake
Unamsikia kabisa mtangazaji akisikitika mpira unapoelekea upande wa goli la "timu yake" na kumlaumu beki aliyesababisha goli kufungwa.
 
Unamsikia kabisa mtangazaji akisikitika mpira unapoelekea upande wa goli la "timu yake" na kumlaumu beki aliyesababisha goli kufungwa.
We ni nzi wa kijani, na umeandika kwa kuongozwa na mahaba. Tulia tu dawa ikuingie vizuri.
 
Shafii hawezi kuwa simba namjua toka mdogo yanga ikifungwa hali
 
We ni nzi wa kijani, na umeandika kwa kuongozwa na mahaba. Tulia tu dawa ikuingie vizuri.
fair play and fair broadcasting msingi wake ni shule kubwa kwa wa wadau wote. Una ka-certificate/ka-diploma wapi na wapi
 
Kuna shaffih Dauda yaani hafai kabisa, siku simba ikifungwa anakuwepo studio kwa kuisemea mabaya, siku ikishinda aonekani au akiwepo hafanyi uchambuzi! Leo simba kashinda ametoa tu matokeo akaamia sakata la nyoso!
Yule hafai hata kuchambua rede,eti still bado,sheeenzi
 
Back
Top Bottom