kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ni pale mtangazaji wa mpira redioni anapoacha kuutangaza mpira unavyochezwa uwanjani badala yake anatangaza mpira wa upande mmoja anaoushabikia (timu yake) na kuwanyima ukweli wasikilizaji wake juu ya kile kinachoendelea uwanjani kwa wachezaji na timu zote uwanjani. Na kwa bahati mbaya anafanya hivyo kwenye redio ya umma inayoendeshwa kwa kodi za mashabiki wa timu zote nchini.
Hizi ni dalili tosha kuwa tasnia ya habari pia ina wafanyakazi ambao hawajaiva vizuri wasioweza kujiongeza. Kama wewe una mahaba yaliyopitiliza kwa timu yako nenda kafanyekazi kwenye chombo cha habari cha timu yako, vinginesho anzisha chombo chako cha habari ujimwage huko ili wananchi wapenda mpira wa miguu wawe na hiari ya kukusikiliza huko au la.