Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe kuchukuliwa hatua

Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe kuchukuliwa hatua

Hapo Masanja na Kitenge wana windwa!
Hivi TCRA nani kawambia usomaji wa magazeti kwa mbwembwe ndio shida za watanzania? Hivi TCRA ujinga mtaacha lini? Hivi Nape kwanini umeamua kuminya uhuru wa habari? Kwani kuna kosa gani watu kusoma kwa mbwembwe? Kwanini mnataka kila station iwe kama TBC FM!

Huu ni upumbavu kabisa badala ya kushughulikia sukari nyie mnashughulikia vyombo vya habari
 
Uhuru wa habari na vyombo vya habari ni mfupa mgumu sana ndani ya taifa hili. Media capture ni jenga kwa taifa.
 
Hapana. Hawa wasomaji wanavunja miiko ya utangazaji. Ni Tanzania pekee unaweza kukuta ujinga kama huu. Hii ndiyo hasara ya kuokoteza wapiga domo mitaani na kuwafanya watangazaji. Elumi, ndogo, ufahamu mdogo, eti mtu anapewa utangazaji kwa sababu tu anajua kuzungumza kwa haraka haraka.
Hakuna sheria yoyote ya utangazaji inavunjwa waandishi kusoma magezeti kwa mbwembwe au mikogo. Pia ukiacha tabia ya kusifia watawala kulikopitiliza uandishi wa habari uliopo Tanzania hautofautiani na sehemu nyingine yoyote duniani ambako sekta ya uandishi wa habari inaongozwa na mahitaji ya soko huria.
 
Jamaa ni wapuuzi sana yani..

Huwa inatokea mazingira sometimes unakuta redio wapo wao.. Ni aibu..

Yani watu wanatumia resources zao na muda.. Wana risks wakati mwingine maisha ili kusaka habari.. Wanazichapisha na kusambaza magazeti kwa gharama halafu mtu tu studio anasoma gazeti kama nini sijui.. Wapuuzi..

Hawa wamecheleweshwa tuu.. Mimi ningekuwa naandika magazeti au najihusisha huko ningewashitaki mapema tu kabla ya hao TCRA hawajawafikia... Wanacheza na kazi za watu kabisa live live for their own benefit and gain...

Kwa usomaji wao ule gazeti linapoteza thamani.. Hata kama ni hard news inageuka kuwa satire tu... Hovyo sanaa
Kwanza hard news ni nadra sana katika magezeti karibia yote ya sasa ya bongo, pia ukiona kampuni za magazeti wako kimya kutokana na magezeti yao kutumika redioni ujue hilo ni suala lenye manufaa zaidi kwa kuliko hasara. Kama wangekuwa hawataka magezeti yao kutumika hivyo wangeshaenda mahakamani au kulalamima kwa TCRA au Waziri.
 
Hao TCRA wamekosa chakufanya kabisa
 
Na wale wanaosoma kwa uzembe uzembe kama Uhuru FM je?
 
Na kitenge hii gabari ataisoma kwa mbwembwe kmmk.
 
Kwanza hard news ni nadra sana katika magezeti karibia yote ya sasa ya bongo, pia ukiona kampuni za magazeti wako kimya kutokana na magezeti yao kutumika redioni ujue hilo ni suala lenye manufaa zaidi kwa kuliko hasara. Kama wangekuwa hawataka magezeti yao kutumika hivyo wangeshaenda mahakamani au kulalamima kwa TCRA au Waziri.

Kwa maandisha haya hakika nakwambia, hata Tembo akiwekwa pale katikati ya uwanja wa Lupaso hautaweza kumuona.

Ingekiwa ni wewe ungelalamika kwa njia ipi? Acha regulator apambanie...

Kosa huwa linatafutwa katika namna na hali ya maisha yako ilivyo... Ili saa na wakati ukifika...
 
Pia wazuie TBC na CH 10 kubagua magazeti. Watasoma magazeti ya dola na chama tu afu watatuambia ndo yalyomo magazetini
Wanasahau magazeti private kama citizeni na Nipashe
 
Hakuna sheria yoyote ya utangazaji inavunjwa waandishi kusoma magezeti kwa mbwembwe au mikogo. Pia ukiacha tabia ya kusifia watawala kulikopitiliza uandishi wa habari uliopo Tanzania hautofautiani na sehemu nyingine yoyote duniani ambako sekta ya uandishi wa habari inaongozwa na mahitaji ya soko huria.
Muhimu: sheria ya utangazaji siyo sawa na miiko ya utangazaji na miiko siyo sheria. Utangazaji wa Bongo ni wa kiwango cha chini mno mno kiasi ambacho naweza kusema siyo utangazaji bali ni upiga porojo na udalali. Anyways, hili siyo kila mtu anaweza kuliona ndiyo maana bado wasikilizaji ni wengi. Umewahi kumsikiliza Masoud Masoud? Basi huyu ndiye mmoja ya watangazaji ambao naweza kuwasikiliza. Kitenge sijui na kina Zembwela katu siwezi.
 
Nakubaliana na wewe kwamba utangazaji wa bongo uko chini sana hasa kwa kuzinagatia maslahi na mahitaji mapana ya taifa lakini hao wakina Zembwela, Kitenge, Mwijaku n.k hakuna sheria au miiko yoyote wanayovunja kwa aina yao ya utangazaji. Ni kwamba haina tija kubwa tu.
 
Back
Top Bottom