Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe kuchukuliwa hatua

Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe kuchukuliwa hatua

Tcra nani kawaambia mahitaji ya watanzania na kero kubwa kwao ni wasoma magazeti kwa mbwembwe? Wazee wa tuma ile hela mmeshindwa kuwakomesha, bando ziko juu ila hili hamulioni bali mnaoma wasoma magazeti
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itawachukulia hatua baadhi ya watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe huku wakiongezea baadhi ya ya vitu wakati wa usomaji.

Hayo yameelezwa na Meneja Huduma za Utangazaji, Andrew Kisaka katika mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini.

Swahili times
kitenge na mambo yake ya dursalaam...ndo nini!!
 
Hawa nao wamekosa kazi ya kufanya!
Wakala wa serikali ndiyo jukumu lake hilo? kama mtu hupendi ujinga hama stesheni stress nyingi sana ujinga unaburudisha, watuache sukari bei gani vile?
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itawachukulia hatua baadhi ya watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe huku wakiongezea baadhi ya ya vitu wakati wa usomaji.

Hayo yameelezwa na Meneja Huduma za Utangazaji, Andrew Kisaka katika mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini.

Swahili times
Nchi ikiendeshwa na watawala wa hovyo, hata taasisi zake nyingi huwa za hovyo
 
Waache tu watu huru, kuna wapumbavu wanaofurahia usomaji wa magazeti wa kipumbavu wa akina Maulidi Kitenge na wenzake.
 
Kwa nini??
Chances are kuna mchepuko wa mmoja wa hao wenye vyeo TCRA kamwambia Bwana wake kuwa anakerwa na mbwembwe Bwana nae kaamua iwe sheria kutokusoma kwa mbwembwe.

Sheria za nchi hii ni kwa mujibu wa utashi wa mwenye mamlaka.
 
Hapana. Hawa wasomaji wanavunja miiko ya utangazaji. Ni Tanzania pekee unaweza kukuta ujinga kama huu. Hii ndiyo hasara ya kuokoteza wapiga domo mitaani na kuwafanya watangazaji. Elimu, ndogo, ufahamu mdogo, eti mtu anapewa utangazaji kwa sababu tu anajua kuzungumza kwa haraka haraka.
 
Tcra nani kawaambia mahitaji ya watanzania na kero kubwa kwao ni wasoma magazeti kwa mbwembwe? Wazee wa tuma ile hela mmeshindwa kuwakomesha,bando ziko juu ila hili hamulioni bali mnaoma wasoma magazeti
[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Tanzania kila kitu ni kituko. Mimi huwa sisikilizi hawa wasoma magazeti hata siku moja.

Jamaa ni wapuuzi sana yani..

Huwa inatokea mazingira sometimes unakuta redio wapo wao.. Ni aibu..

Yani watu wanatumia resources zao na muda.. Wana risks wakati mwingine maisha ili kusaka habari.. Wanazichapisha na kusambaza magazeti kwa gharama halafu mtu tu studio anasoma gazeti kama nini sijui.. Wapuuzi..

Hawa wamecheleweshwa tuu.. Mimi ningekuwa naandika magazeti au najihusisha huko ningewashitaki mapema tu kabla ya hao TCRA hawajawafikia... Wanacheza na kazi za watu kabisa live live for their own benefit and gain...

Kwa usomaji wao ule gazeti linapoteza thamani.. Hata kama ni hard news inageuka kuwa satire tu... Hovyo sanaa
 
Back
Top Bottom