Watangazaji wawili wa KYELA FM walioshikiliwa na Jeshi la Polisi waachiwa kwa dhamana Mkoani Mbeya

Watangazaji wawili wa KYELA FM walioshikiliwa na Jeshi la Polisi waachiwa kwa dhamana Mkoani Mbeya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Wanahabari wawili wa kituo cha redio cha Kyela FM, Tumsifu Katina na Emmy Eliud, wameachiliwa kwa dhamana asubuhi ya leo Aprili 15, 2026 baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi tangu jana mchana.

Meneja wa Kyela FM, Lamso Malongo amethibitisha kuwa wanahabari hao kwa sasa wako huru na taratibu za kuwasafirisha kutoka jijini Mbeya kurejea Wilayani Kyela zinaendelea ili waweze kuungana na familia zao.

Sababu za Kukamatwa:
Malongo alieleza kuwa kukamatwa kwa wanahabari hao kulitokana na kipindi walichokifanya mnamo tarehe 9 Machi, 2026 ambapo walikuwa wakisoma na kuchambua habari kutoka kwenye Gazeti la Mwanahalisi. Habari hiyo ilikuwa ikihusu utendaji wa Jeshi la Polisi, jambo lililopelekea polisi kuwaita kwa ajili ya mahojiano kuanzia saa tisa alasiri ya jana kabla ya kuwahamishia jijini Mbeya usiku wa kuamkia leo.
photo_2026-04-15_00-43-52.jpg

photo_2026-04-15_00-44-12.jpg
Hali za Wanahabari na Hatua Zinazofuata
Kuhusu hali zao na kama kuna masharti yoyote ya dhamana waliyopewa, Meneja huyo amesema kuwa watatoa taarifa rasmi (press release) mara baada ya kukutana nao na kufanya mazungumzo ya kina.

Amesema "Tutatathmini hali zao na kama kuna masharti yoyote yamewekwa, tutayaweka wazi. Kwa sasa tunashukuru kila aliyepaza sauti, vikiwemo vyombo vya habari, kwani imekuwa msaada mkubwa katika kuharakisha mchakato huu.”

Pia soma
~
Watangazaji wa Kyela FM walioripoti kuhusu Afande aliyetoa kero kwa Mwigulu 'kutoweka', wamekamatwa na polisi

~ Polisi Pwani wakanusha Mwigulu kumteka Askari aliyetoa kero kwake kuhusu askari mwenzake

~
Polisi ataka kumpasua RPC wa Pwani hadharani Waziri Mkuu amzuia
 
Tyranns yaani Kisa walisoma habari ya polisi aliyemshitaki RPC kwa mwigulu loh nchi ngumu sana hiyo , lakini
Wakisifiwa ruksa 🤷‍♂️
 
Back
Top Bottom