Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Tamka hivi majina ya timu hizi.
Ajax=Ayaks
Internazionale Milan=Intanasional Milano
Sevilla=Sevia
Burnley=Banli
Legia Warszaw=Lehia Vaso'o
Schalke 04=Shak (Nur fia)
Monchengladbach=Monshen'gladbak
Borussia Dortmund=Borushia Dotmund
Sporting Gijon=Sporting Hihon
Swansea=Swansii
Tottenham=Totenam
Anderlecht=Andalek
Brazil=Brasiil
Lazio=Lasio
Juventus=Huventus
Fulham=Fulam
Valencia=Valenshia
....................
Valencia- valenthia
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Thanks . umesema kweli. Maana niliishi Worthing miaka 5.
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Unakuta anasema "professional" yangu ni mwanasheria, pumbavu kabisa😅
 
Hujaelewa nini kinazungumzwa hapa. Ushasasikia watangazaji wa Kiingereza wakitamka Jose Mourinho,Juan Mata au Thierry Henry? Wanatamka kwa jinsi inavyotamkwa kwa lugha za wahusika. Na hapa nazungumzia watangazaji si watu wa mtaani.
Sizungumzii accent, kutamka lesesta badala ya lesta sio accent.
Hao ni watalaam, huku bongo hizo mambo hakuna kutokana na kutojua lugha mbalimbali
 
Hayo maneno ya maeneo ya ulaya na ugaibuni sio issue sana kwana hata wazungu wenyewe wakija kwetu maeneo yetu yanawashinda kutamka kinachoniudhi ni wale wanaoshindwa kutofautisha kati ya herufi L na R kwenye magari mathalani atatamka magali
Tena mkuu inanikera mno. Wazungu, Waarabu na Wahindi wanashindwa kutamka majina yetu hasa ya ASILI, badala ya sisi kuwalazimisha kutamka kama tunavoyatamka tunawafuata wao wayakoseapo na kiaandishi hivohivo. Mfano Idodomya kuitwa Dodoma!
 
Usishangae mkuu hata hao wenye majina hayo walikuja kwetu enzi hizo walishindwa kutamka majina ya maeneo yetu wakaharibu mpaka leo tunataja majina ambayo siyo asili yetu.

Mfano, Tabora, Njombe, Iringa, kwenye mito wameharibu na milima pia.
Kinachoshindikana ni nino kuyarekebisha? Huu ni utumwa wa kifikra.
 
Hiyo mizungu si ndio imetuletea Bagamoyo badala ya bwagamoyo na dodoma badala ya idodomiya? Rufiji badala ya Rupwiy
Kinachotushinda kurekebisha ni nini hasa? Au mpaka haohao waturekebishie!!!???
 
Tusiwalaumu watangazaji kushindwa kutamka majina ya Wazungu, Waarabu na Wahindi kiusahihi. Tujilaumu kwa kuendelea kutumia majina yetu hasa ya sehemu kama yalivokosewa/walivotaka wao.
 
Back
Top Bottom