Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Mkuu Tanzania tunamatatizo mengi sana hilo nalo ni tatizo pia..

Darasa la kwanza mpaka la saba kiswahili mwanzo mwisho, ghafla tu unaanza form one kiingereza mwanzo mwisho hapo ndio mpaka unakua Professa lazima ukariri tu mwisho wa siku ukajibu mtihani.
Jamaa nakupa tuzo kwa kugundua hili tatzo
 
Hayo maneno ya maeneo ya ulaya na ugaibuni sio issue sana kwana hata wazungu wenyewe wakija kwetu maeneo yetu yanawashinda kutamka kinachoniudhi ni wale wanaoshindwa kutofautisha kati ya herufi L na R kwenye magari mathalani atatamka magali
Hii L na R ni janga la taifa. Naona kama wanafanya makusudi maana hata kimaandishi wanaandika hivyo. Hivi somo la mwandiko bado lipo kwenye shule za msingi?
Kuhusu wazungu kushindwa kutamka isiwe kisingizio kwetu. Akishindwa mzungu sio lazima na mwingingine ashindwe. Pia wale watangaza habari ughaibuni hawakosei ovyo. Wakichapia wanaomba radhi.
 
Majina mengine unajifunza kwa kusikiliza wenye majina yao. Mfano Hughes inatamkwa Hyuz sasa utasikia mtangazaji anatamka hugiz/hagiz/hagez
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Umenena mkuu, kuna watu wanaangalia kipaji, ukubwa wa jina nk. Kama uko vizuri unakula kazi.
Mfano, jamaa mmoja ananogesha kipindi cha michezo pale mawingu fm.
Mwingine yupo kipindi cha jioni cha Efm ni comedian fulani hv.
uliishaambiwa watoa fursa hawaangalii vyeti, wanaangalia talent
 
Tamka hivi majina ya timu hizi.

Ajax=Ayaks
Internazionale Milan=Intanasional Milano
Sevilla=Sevia
Burnley=Banli
Legia Warszaw=Lehia Vaso'o
Schalke 04=Shak (Nur fia)
Monchengladbach=Monshen'gladbak
Borussia Dortmund=Borushia Dotmund
Sporting Gijon=Sporting Hihon
Swansea=Swansii
Tottenham=Totenam
Anderlecht=Andalek
Brazil=Brasiil
Lazio=Lasio
Juventus=Huventus
Fulham=Fulam
Valencia=Valenshia
....................
 
..inakera sana hasa ukizingatia kuwa hawa watu wanapata nafasi ya kusikika na wengi...jana nimemsikia yule mtangazaji (mwandishi?) Baby Kabaya kwenye mazishi ya Mzee Mengi akisema...." ....Hizo ni makaburi za familia..." badala ya ..." hayo ni makaburi ya familia..". Wanaonikera zaidi ni wale waosema..Nyimbo hii..badala ya wimbo huu!
Yule nasikia sio mtanzania wa asili.
Kama sio mkenya ni mganda.
 
Ni matamshi tu. Hata watu kwenye Mataifa yenye maendeleo kama Wafaransa na Wajapani wanapata shida na Kiingereza sababu lugha zao zipo tofauti sana.
Huajiri mtu ambaye ni mahiri katika lugha husika. Kwa sisi Kiingereza sio lugha ngeni kiasi hicho.
 
kinachoniudhi ni wale wanaoshindwa kutofautisha kati ya herufi L na R

Hawa mkuu wapo wengi sana, tatizo ukiigiza style ya kuongea lazima kwenye R useme L and viceversa. hasa wale wanaomix kiswaenglish
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Dingi hayo majina si yetu, hata wewe unayajua machache tena kwa kuunga unga. Jina la kijerumani, mtangazaji kijerumani hajui. Wao kwenye v wanatamka f, w wanatamka v.
Matamshi ya lugha yanaathiriwa na lahaja (variant) pia lafudhi ( accent).
Wamarekani na waingereza wote wanatumia kiingereza lakini kuna baadhi ya maneno wanatamka tofauti.
 
inatamkwa hov mabano u ?

bora aliyesema hove
Hapo nadhani kamaanisha kuwa hiyo u unaimezea unakuwa ni kama unasema hov!! Sasa ukiweka hyo u mwisho inakuwa hovu ambayo unakuwa umetamka kindengereko zaidi!!

Wandengereko mnisamehe ndugu yenu.
 
Back
Top Bottom