Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Kwa kweli kama unajifunza lugha ya watu au hata majina ni lazima uyatamke kama yanavyotamkwa na wenyewe (sio kwa wazungu tu)
Sasa unashuka airport halafu unataka kwenda mji uliokuwa unajua linatamkwa hivyo nakuapia dereva hatakuelewa na itabidi akupe kalamu uandike [emoji3][emoji3]
 
Big up bro japo kuna watu watapambana na wewe kwa sababu chuki yao dhidi ya hii lugha tamu mdomoni ni kubwa mpaka yeyote anayeiongea anakuwa adui na ataitwa anajifanya [emoji16]
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
 
Yupo sawa kabisa ticha wako
RRONDO nina mwalimu mmoja wa kizungu eti alinifundisha kutamka. Lester.

Ana asili ya kimasai lakini mama mdiye mzungu.. ila nadhani anajua kizungu maana namwamini.
 
"Wulvs" bosi ama "wulvhampton" nimetumia njia mbadala kurahisisha. Kwa msaada zaidi tafuta Kamusi ya Oxford.
Bado sijaona kosa,kujaribu kutamka neno kwa lafudhi ya kingereza au kifaransa au kihispania kunaweza kupoteza maana ya neno,mfano aliyekuwa kocha wa man u anaitwa jose lkn wenyewe wanaita hozee,na bado kuna watu wanaitwa jose ila huwezi mwita hozee akakuelewa,,,laurent mfaransa atasema loraa na wewe mswahili unasema loraa (kifaransa)
 
Utasikia mtangazaji wa TV wa Bongo akisema, "Yule supermodel wa Uingereza, Naomi Kampbeli..."
Duuuh, majanga!
Naomi Campbell [tamka= Naomi Kembo]
 
Kuna matako mmoja yuko Generation FM alikuwa anasema "boss wa cash money butt man amekutana club na Lil Wayne"
Hapo kwenye butt man alikua anamaanisha Birdman.
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Arsenali,Evatoni,Livepuli
 
Vikta Lindelofu
Victor Lindeloff [tamka: Victa Linda-love], yerewiiii!
 
Wajapani waliligundua hili ndo maana majina yao yote yana vowels. Tanakuwa mepesi kutamka
Mfano.
Honda
Yamaha
Toyota
Nagasaki
Kiyosaki
Shinji Kagawa
Bolo Young (young ni kingereza lakini hilo bolo ni la kijapani)
Bolo Yeoung ni Mkorea Kusini Sio Mjapani......Wajapani majina yao hayana tofauti sana na Wabantu.
 
Utasiki Litangazaji linatamka jina la Bob Marley "Bobu Male" Badala ya "Bob Mali"
 
Sasa kama iliishia form 4 ya div 4 unatagemea huyo ndugu yako atatamkaje hayo maneno na hata kujua vichache tu kuhusu hayo mambo anayoyatangaza??
Chuo chenyewe kasoma Ilala Bungoni au Eagle kwa miezi 6 sasa kuna kipya unakitarajia hapo??
Jana nimemsikia mmoja ktk kipind cha michezo akidai Tottenham wamekiwakisha katika jiji la Ajax walipocheza na Ajax, nikajiuliza anataka kusema walicheza kule Canada ambako katika jiji la Ontario kuna town inaitwa Ajax?
Kupata alama pungufu baada ya kuhitimu elimu ya kiwango fulani isiwe sababu jamani. Kuna kujiongeza pia. Matumizi ya smart phones, tv na redio vinasaidia sana kwenye taaluma ya habari. Kuuliza pia sio ujinga. kama hujui, huna uhakika unaweza kuuliza hata huku JF na utasaidika na kujifunza. Uvivu unachangia kwa asilimia kubwa.
 
Back
Top Bottom