Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Valencia- valenthia
 
Thanks . umesema kweli. Maana niliishi Worthing miaka 5.
 
Unakuta anasema "professional" yangu ni mwanasheria, pumbavu kabisa😅
 
Hao ni watalaam, huku bongo hizo mambo hakuna kutokana na kutojua lugha mbalimbali
 
Hayo maneno ya maeneo ya ulaya na ugaibuni sio issue sana kwana hata wazungu wenyewe wakija kwetu maeneo yetu yanawashinda kutamka kinachoniudhi ni wale wanaoshindwa kutofautisha kati ya herufi L na R kwenye magari mathalani atatamka magali
Tena mkuu inanikera mno. Wazungu, Waarabu na Wahindi wanashindwa kutamka majina yetu hasa ya ASILI, badala ya sisi kuwalazimisha kutamka kama tunavoyatamka tunawafuata wao wayakoseapo na kiaandishi hivohivo. Mfano Idodomya kuitwa Dodoma!
 
Usishangae mkuu hata hao wenye majina hayo walikuja kwetu enzi hizo walishindwa kutamka majina ya maeneo yetu wakaharibu mpaka leo tunataja majina ambayo siyo asili yetu.

Mfano, Tabora, Njombe, Iringa, kwenye mito wameharibu na milima pia.
Kinachoshindikana ni nino kuyarekebisha? Huu ni utumwa wa kifikra.
 
Hiyo mizungu si ndio imetuletea Bagamoyo badala ya bwagamoyo na dodoma badala ya idodomiya? Rufiji badala ya Rupwiy
Kinachotushinda kurekebisha ni nini hasa? Au mpaka haohao waturekebishie!!!???
 
Tusiwalaumu watangazaji kushindwa kutamka majina ya Wazungu, Waarabu na Wahindi kiusahihi. Tujilaumu kwa kuendelea kutumia majina yetu hasa ya sehemu kama yalivokosewa/walivotaka wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…