Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Ndugu yangu nilisikia siku moja jina la kocha wa Man U likitamkwa redioni, nusura nijifiche uvunguni. Pamoja na kwamba linaonekana gumu lakini huwa linatajwa tajwa na linatamkwa kiurahisi tu "Sosha". Siku hiyo lilitamkwa "soskajei" kitu kama hicho
Ila hilo jina gumu sana
 
Watangazaji wanapaswa kujiongeza kiasi, pengine wangejaribu kufuatilia vyombo vya habari vya nje angalau wakapata kujifunza majina ya viongozi wa kimataifa, mitaa, timu za mipira na wachezaji wake na mambo mingi mengine mfano wa hayo, hicho kingewawezesha kuwa na uweledi na ladha katika kazi yao.
 
Hao wa huko wanatamkaje Mwanza, Morogoro? Kigurunyembe? Nk nk? Kama haukai huko utajuaje kuwa inatamkwa hivyo? Haifundishi darasani hapa Tanzania hiyo! Yale yanayofundishwa darasani hapa Tanzania, wanajua jinsi ya kuyatamka. Utajuaje kuwa Gaborone inatamkwa "Haborone" kama hujawahi kuishi ama kufika Botswana?
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
 
Jina la kwanza tamka lilivyo andikwa la pili kwa lugha ya Dutch, Kijerumani, Afrikaans helufi S inatakiwa Z hivyo tamka Zeedowf
Klarens Seidof [emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna dogo yuko Clouds FM kipindi cha Sports, huwa anaripoti kuhusu Basketball baadhi ya siku, anajitahidi sana kuyatamka majina ya wale wachezaji na teams inavyopaswa.

Ila kuna majina hayatamkiki aisee.
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Ni kweli makosa ni mengi sana kutamka majina ya watu, vitu, maeneo nk....lkn ndio watu wenyewe hawa(wtz)hawajui pa kuweka R na L kwenye lugha yao..... hatari sana!
 
Hata hapo Nairobi wamasai halisia walikuwa wanapaita Nairobai. Kwa mwingereza ai ndio anavyotamka i. Ikawa Nairobi. Kwa huko Scandinavia wanatamka London kama inavyoandikwa ila mwingereza yeye anatamka Landan, kwa mfano.

Ni sawasawa kama wajerumani walivyoshindwa kutamka neno Bwagamoyo na wakaondoa herufi "W" na watanganyika tukakubali iiwe hivyo na mji uitwe Bagamoyo.

Wazungu wengi nao wanamatatizo na baadh ya herufi na mojawapo ni herufi "W".

Hilo eneo la Bwagamoyo lilikuwa na maana yake na hilo neno, yaani watumwa wote walokuwa wakifika hapo kutokea bara waliambiwa wabwage mioyo yao hapo.

Ilikuwa ni sehemu ya kuaga Afrika kwenda utumwani huko uarabuni
 
Back
Top Bottom