GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Njooni huku Uswahili kwetu mkute Misiba ya Watani zangu Washamba tupu akina Wahaya, Wanyiramba, Waha, Wanyaturu, Warangi, Wakara na Wanyamwezi ikitokea halafu mtuone Watu wa Mara (Musoma) tunavyoinogesha kiasi kwamba hata Marehemu mwenyewe sometimes huwa anatabasamu Jenezani alipolala.
Misiba ya Kitajiri imekaa Kishamba mno kwani mnajifanya mna Uzungu Uzungu (Usasa Usasa) kiasi kwamba unakuta Ukimya mwingi tu Umetawala hapo Msibani. Misiba mizuri ni ile ambayo Watani wanapita huku na kule kukusanya Michango na hata Kuwapiga Madongo ya kati na ya uhakika wanafamilia kama walikuwa wanaishi Maisha tofauti na wengine katika Jamii.
Niliwahi kuhudhuria Msiba wa Washamba Wahaya (Watani) zangu na Wazanaki wote na hata Makabila mengine ya kutoka Kwetu Mkoani Mara tulienda na nakumbuka Marehemu alikuwa anatakiwa Kusafirishwa kwenda Kagera ila kukawa na Uzito wa Watu (hasa Wahaya Kuchangia) na tulichoamua kukifanya ili Hela ipatikane tukaanza sasa kuwapiga Madongo Wahaya Matajiri tuliokuwa tunajua tabia zao na Wao kwa Kutuogopa wana Mkoa wa Mara tukawa kila tunayemkaribia tukitaka tu kumpiga Dongo haraka sana wanatuwahi Kutunyamazisha na wanatoa Hela.
Ndani ya Saa mbili zilipatikana Fedha zote zilizotakiwa na tulichokifanya ni kwenda kukata Tiketi ya Ndege ya Marehemu na Kiasi kilichobakia tukampa Mjane na Maisha yakaendelea. Kuna Watu mmejaa na Ushamba mnadhani Watani wakija Misibani kwenu wanakuja Kula au Kuchota Fedha zenu za Msiba.
Hakikisheni huu Utamaduni wa Utani Misibani usiachwe kwani una Faida Kubwa mno kuliko Watu wengi muwazavyo.