Watani zangu wasukuma hebu punguzeni matumizi ya vyakula, mnaharibu

Da mnatisha
 
Mimi sikujua kama kunaubweche umepikwa nikadili na ugali
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hatari aisee
Nimecheka sanaaaaa!! Huko ndo ukandani mkuu, huo si utaratibu wa wasukuma tu, utaratibu wa wakanda ya ziwa karibu woteee, kuanzia ukerewe, kwa wakara, wazinza, wajita, wakurya na wengineo.
 
Kuna mmoja yuko huko Ulaya,asubuhi anaamka na viporo vya wali kama hana akili sawasawa,wazungu wanabaki kumshangaa wanatikisa vichwa.
 
Kuna mmoja yuko huko Ulaya,asubuhi anaamka na viporo vya wali kama hana akili sawasawa,wazungu wanabaki kumshangaa wanatikisa vichwa.
Ha ha haaa.
Harusi huwa unaanza na Ugali then ukiutandika sawasawa, baadae sasa wali unakuja kama Tunda, unaweza kuwa unatoa machozi tu na nia ule lkn hali ya Tumbo inakuwa hairuhusu, yaani roho i radhi mwili u dhaifu.
 
Na bado ungekoma kama ungeendelea kukaa angalau wiki,,

Kuna uji wa asubuhi unaitwa nyuka.
Alafu baada ya uji unaletewa mahindi ya kuchemsha na
viazi vya kuchemsha"manumbu"na mihogo"mbute"

Tunawafundisha kula watoto wetu wafupi ili mrefuke,
Hahaha! Daah umenikumbusha boarding shuleni hapo zamani kidogo,ule uji wa saa nne tulikuwa tunauita Nyuka! Sukari ilikuwa ni ya kuitafuta kwa tochi.

Lakini ajabu ni kwamba msukuma alikuwa anaweza hata kumaliza lita saba na akaenda darasani bila kusinzia.
 
Ha ha haaa kula lazima, haswa quantity
 
cc Pascal Mayalla
 
nikiwa kama msemaji mkuu wa wasukuma nasema hivi sisi ndio kawaida yetu kama huyo rafiki yako alishindwa kukwambia ukweli basi ndio tulivyo... Halafu sisi hatuna kijiji bali popote kambi..

Pole sana mkuu hata mimi ilinitokea hii.
 
Hakika hii ndo ilionitokea mimi mkuu[emoji28][emoji28][emoji28]unamaliza kula inakuja pati2 shehena za sinia za bweche
mbona unesahau picha sasa! wenyeji na watani zetu wa kanda maalumu dar, moro, pwani, tanga, z'bar msituletee ubahiri wenu bhana. bise tulibegereja polapole! View attachment 1112411
 
Hakika nilikula siku hiyo tangia nizaliwe sikuwai asubuhi tulikula wali nyama ya kuku mchana ugali nyama ng'ombe aliebanikwa na maziwa mgando sijakaa sawa mbuzi akavutwa na kamba shingoni nakaribishwa kua achijwe usiku full mbuzi mchezo wao wakuanzia ugali tayari nilikua nisha usoma[emoji3][emoji3] nilikula ugali kwa kufinyafinya tu nimesubili bweche haa haaa
nikiwa kama msemaji mkuu wa wasukuma nasema hivi sisi ndio kawaida yetu kama huyo rafiki yako alishindwa kukwambia ukweli basi ndio tulivyo... Halafu sisi hatuna kijiji bali popote kambi..

Pole sana mkuu hata mimi ilinitokea hii.
 
Ha ha haaa, kwa mgeni usukimani mchezo wa kuletewa ugali mwanzoni ukiutegua utapiga ubweche na nyama nyingi baade, ila ukiufakamia ugali, baadae tunda (wali) likija utatoa macho kwa mshangao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…