Mama twende Usukumani basi
Mama twende Usukumani basi [emoji23][emoji23]
Haya maisha ya kalikuleta hata wakati wa msosi ndio shida wewe umezoea 1/8 ya kilo ya nyama wali 1/4 mara nyingi hizi jamii za kuongea kiswahili saaana wanakula saa 11 jioni ndio chakula cha mchana na usiku , ulizoea kupiga ndefu a.k.a goli kwa goli
Kijana KULA UKUE ndio maana urefu ukanda wenu mrefu saana ft4 kama ulienda kuchukua mahari ya dada yako Sawa mbegu mmepata ila kama unaoa utaharibu ukoo. Anyway endelea
Sasa ungesogea kwa majirani zao wakurya hapo mara ndo ungezimia.. Ila uzuri wa kanda ya ziwa watu wanapiga kazi kweli kweli tofaut na hawa washindia burger na chips wa Dar.
Ni kawaida hiyo kwetu tuna vyakula vya kututosha , tukirudi makwetu na madigrii yetu tunachunga, tunakamua. Wewe unafikiri hiyo miili yetu mikubwa inakuja kwa kula half cake na fursana? Karibu tena mkuu
Jamaa wako vizuri sana kwenye kukirimu wageni nakumbuka nilienda mkoa wa Tabora sehemu moja inaitwa URAMBO nilimtembelea rafiki yangu msukuma aisee nilipokelewa na ukarimu mkubwa kuliko hata ninavyopokelewa nikienda kwa bibi yangu mzaa Baba
Nakumbuka chakula tulichokuwa tunakula
Asubuhi - Tunakula Ugali wa Donna na mlenda / samaki wa kavu huku mnashushia na mtindi kisha tukimaliza ugali linaletwa Sinia limejaa viazi vitamu mnashushia na Maziwa Fresh yaliyotoka kukamuliwa mda huo huo
Mchana - Dona/ Ugali wa mtama mboga mlenda na nyama
Usiku nilipikiwa wali na kuku mzima nikaletewa Chungu kizima peke yangu aisee nilikula nyama ya kuku mpaka nikashiba huku nashushia Maziwa ya Mgando
Wasukuma nawapa big up 100% mnajua sana kukirimu wageni na kuwahudumia safi sana
Hee asubuh ugali+mlenda+visamaki+mtindi halafu muda huohuo Viaz na maziwa fresh?Saluti
Mnajifanya wajuaji kumbe mnaharibu
Wakuu habari zenu leo nitaongelea hawa watani zangu wasukuma japo mimi ni mkazi wa morogoro, juzi juzi tulikua kijijini kwao na rafikiangu kwakweli tulipokelewa vizuri familia nzima ilikua na furaha ni familia yenye watu wengi tulionekana kua wageni kweli kweli niliona jogoo wawili wakubwa wamefungwa kamba
Badae rafikiangu alinitembeza kwenye mashamba yao hadi kwenye mbuga za mipunga jioni saa1 tulirudi nyumbani nikiwa nauchovu nikapewa maji ya kuoga saa2:30 msosi ulikua tayari na nilikua na njaa kinoma tulikua tumekaa pembeni kidogo na mwenzangu tukiwa tunachezea simu kupoteza mda alikuja dada mmoja akatukaribisha tukale,
Wasukuma wanadestuli ya kula kwa pamoja wanaume peke yao na wanawake nawao pia upande wao, upande wetu wanaume zilikuja sahani mbili za ugali kubwa na bakuli zilizo jaa nyama na maziwa mgando kwa pembeni, tukala navile mimi navoyapenda maziwa mgando nilikula sana, sasa mimi hapo mawazo yangu yalinituma nimalizie nyama niliokua nmeshikilia mkononi nitoshe
chakushangaza walikuja wadada watatu kutoka kule kwenye upande wa wanawake wakachukua vyombo vyote[emoji38][emoji38][emoji38] badae walikuja kiupya na sinia zilizo jaa nundu za ubwabwa(ubweche) na mabakuli makubwa yaliyojaa nyama za kutosha na soda moja moja kila mtu dah nilibaki naangalia tu maana mwanzo nlikua nmefukia vyakutosha rafikiangu akaniambia mbona umepoa tuendelee[emoji38][emoji38] niliutamani ubweche niligusagusa rakini sikua na namna, noma sana
Wasukuma nawapongeza mnamapokezi mazuri kwa wageni ila kwenye chakula hua mnaharibu maana najua chakula kilichobaki ni kingi mno isitoshe na asubuhi tulipikiwa chakula kingine nundu za ubweche.
=Exalioth
Msukuma bora umpikie ugali kuliko vichapati, utamfanya ashinde njaa.Sasa wakija uku mjini aaubuhi si chapati 12+supu+maziwa fresh+ maji makubwa