Uzuri wao wanakula ila wanalima kama trektaMsukuma bora umpikie ugali kuliko vichapati, utamfanya ashinde njaa.
Hatuna njaa kama vikabila hivi vidogo vidogo.Mnajifanya wajuaji kumbe mnaharibu
Wakuu habari zenu leo nitaongelea hawa watani zangu wasukuma japo mimi ni mkazi wa morogoro, juzi juzi tulikua kijijini kwao na rafikiangu kwakweli tulipokelewa vizuri familia nzima ilikua na furaha ni familia yenye watu wengi tulionekana kua wageni kweli kweli niliona jogoo wawili wakubwa wamefungwa kamba
Badae rafikiangu alinitembeza kwenye mashamba yao hadi kwenye mbuga za mipunga jioni saa1 tulirudi nyumbani nikiwa nauchovu nikapewa maji ya kuoga saa2:30 msosi ulikua tayari na nilikua na njaa kinoma tulikua tumekaa pembeni kidogo na mwenzangu tukiwa tunachezea simu kupoteza mda alikuja dada mmoja akatukaribisha tukale,
Wasukuma wanadestuli ya kula kwa pamoja wanaume peke yao na wanawake nawao pia upande wao, upande wetu wanaume zilikuja sahani mbili za ugali kubwa na bakuli zilizo jaa nyama na maziwa mgando kwa pembeni, tukala navile mimi navoyapenda maziwa mgando nilikula sana, sasa mimi hapo mawazo yangu yalinituma nimalizie nyama niliokua nmeshikilia mkononi nitoshe
chakushangaza walikuja wadada watatu kutoka kule kwenye upande wa wanawake wakachukua vyombo vyote[emoji38][emoji38][emoji38] badae walikuja kiupya na sinia zilizo jaa nundu za ubwabwa(ubweche) na mabakuli makubwa yaliyojaa nyama za kutosha na soda moja moja kila mtu dah nilibaki naangalia tu maana mwanzo nlikua nmefukia vyakutosha rafikiangu akaniambia mbona umepoa tuendelee[emoji38][emoji38] niliutamani ubweche niligusagusa rakini sikua na namna, noma sana
Wasukuma nawapongeza mnamapokezi mazuri kwa wageni ila kwenye chakula hua mnaharibu maana najua chakula kilichobaki ni kingi mno isitoshe na asubuhi tulipikiwa chakula kingine nundu za ubweche.
=Exalioth
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Umenkumbusha Dutwa moja hyo pande za Simiyu ni nouma, nilikaa siku tatu niliona kama mwaka yaan, tulikuwa na mnyamwez wangu mmoja hvi daaah ni hatar tupu hatutakuja sahau kamwe, asubuh unaletewa ugali mkubwa na dagaa hawana hata mafuta ni nyanya na chumvi tuu, yaan hapo wamekustah sana mana ni mgeni , msosi night sasa ni amsha, mnaanza kugonga ugali wa adabu alaf game ikiisha inakuja round ya wali, sisi mda huo tushashiba kitambo ila wenzetu wanagonga mpak punje ya mwisho...
Ikifika sa 10 usku wanaamshana kwenda kupiga jembe mpak ngoma 12 join ndo wanarejea..Hatar sana, wanawake wa kule hawana taabu kabisa yaan wao wanajifungulia hata njian, sio wa mjin kati ya wanawake 10 wanaojifungua wanane lazima wafanyiwe upasuaji..sababu ya ukaji wa chips
Na karanga. aelewe pwani kuna njaa..Na bado ungekoma kama ungeendelea kukaa angalau wiki,,
Kuna uji wa asubuhi unaitwa nyuka.
Alafu baada ya uji unaletewa mahindi ya kuchemsha na
viazi vya kuchemsha"manumbu"na mihogo"mbute"
Tunawafundisha kula watoto wetu wafupi ili mrefuke,
Upo sahihi kabisa wasukuma ni tofauti na makabila mengine..Hata akiwa masikini kwenye chakula utakula mpaka utakimbia.Shida inakuja hawa dada wa kisukuma wakiolewa na makabila mengine ya bajeti huwa wanapata shida sana hawajazoea vyakula vya bajeti😀😀😀, basi akirudi kwao wanadhani mwanao alikua anateswa kwa kupungua kumbe mjini wanaenda kibajet bajeti😀utatafuta mapungufu yote ya wasukuma lakini kwenye ukarimu wa chakula ni namba moja siyo wachoyo hata kam ani maskini alichonacho anakukaribisha kwa dhati kabisa
Hakika hii ndo ilionitokea mimi mkuu[emoji28][emoji28][emoji28]unamaliza kula inakuja pati2 shehena za sinia za bweche
Nakumbuka juzi kati tulienda kumpa pole nyumbani jamaa yetu alikua amefiwa pale ni wasukuma...bwanaah weeh ile tumefika hatujakaa sawa tunaona sahani zilizojaa karanga na ndizii za kufa mtu na soda...tukapiga tukajua imeisha Aiseeh yalikuja mayai kama 200 hivi yamechemshwa waliokua na uroho tukapiga Yakatushinda...Tuliwaachia mayai yao Aiseeh[emoji3][emoji3][emoji3]
Wabena ndio wanashikilia rekodi ya ukarimu Tanzania.Me nadhani ni kabila pekee lenye watu wakarimu nchini Tanzania
Trust me, kwa ukarimu na uaminifu Tanzania hakuna kama wasukuma!Me nadhani ni kabila pekee lenye watu wakarimu nchini Tanzania
Mzee avatar yako hatariHatuamini kama ‘ubweche’ ni chakula cha kushiba bali ni ladha tu, so huwa ni muhimu kuanza na ugali kama stata kisha ubweche hasa siku za ugeni au tukio..... halafu usiseme ni uharibifu kwa maana hakuna namna yoyote ile kuwa ubweche unatupwa.
Sisi huku hatuli mavtu magumu kama hayo.mbona unesahau picha sasa! wenyeji na watani zetu wa kanda maalumu dar, moro, pwani, tanga, z'bar msituletee ubahiri wenu bhana. bise tulibegereja polapole! View attachment 1112411
[emoji16][emoji16][emoji16] Dah !!!Ha ha haaa.
Harusi huwa unaanza na Ugali then ukiutandika sawasawa, baadae sasa wali unakuja kama Tunda, unaweza kuwa unatoa machozi tu na nia ule lkn hali ya Tumbo inakuwa hairuhusu, yaani roho i radhi mwili u dhaifu.