Kijana amemaliza degree yake karudi mitaa aliyokulia, yupo bize kuomba kazi na kutembeza bahasha bila mafanikio, kujitolea kwenye taasis kwa mshahara wa laki 1, n.k. Hawezi kufungua sehemu ya kunyoa nywele, kuwa seremala, kuuza mgahawa, n.k. kuna hofu ya watanionaje
Mchezaji wa mpira, msanii, muigizaji, n.k, alikuwa na mfanikio makubwa kapanga nyumba nzuri, gari kali, anavaa fresh, n.k. ghafla soko linamstaafisha, anaendelea kuishi maisha yale yale ya gharama pesa zinaisha, anaanza kukopa mpaka hakopesheki, hofu ya watanionaje ipo kwa kuogopa kuishi maisha ya chini, hakufanya uwekezaji wa maana akiwa kwenye ubora wake kinachobaki ni kuwa mpiga vizinga, uraibu wa madawa ya kulevya, punda wa kubeba madawa, uhalifu, n.k. anaona soo kufanya shughuli za kawaida kwasababu anajiona staa,
Mfanyabiashara alikuwa na mafanikio makubwa ghafla kapigwa na kitu kizito, jawezo kuishi maisha ya chini anaogopa kuchekwa, anaendelea na lifestyle ile ile kutembelea gari linalohitaji mafuta mengi, kuweka heshima bar, kusomesha watoto private za milioni 3, n.k. anakopa pesa aingize kwenye biashara lakini pesa hizo zinaishia kwenye maisha yake ghali kwasababu kakataa kuishi maisha ya chini, matokeo yake anakuwa mdaiwa sugu, kwenye biashara anataka kurudi kwa kasi badala ya kidogo kidogo, biashara zenye faida kidogo kidogo haziwezi kwasababu inabidi ajibane, matokeo yake anaingia biashara haramu za faida chap chap anapigwa na kitu kizito zaidi