Watanionaje...? Itakulaza njaa

Watanionaje...? Itakulaza njaa

Nimekumbuka mbali sana....nilikuwa na deli langu la keki ghafla demu niliyemaliza naye sekondari akaniona...nilitamani nitupe deli Ila nikajikaza tu
Ila sasa mambo yamebadilika nimepiga hatua na wala simuwazi mtu tena kwa niliyoyapitia
😹😹😹 umenichekesha
 
😹😹😹 ana dhambi sana, alitaka kukubunja moyo.!!
Na kweli alifanikiwa maana ilibidi nibadili location kabisa....nikawa nauzia maeneo ya mbali...maana nahisi alienda kumwambia ex wangu kwakuwa alikuwa shoga yake
 
Ushauri: Always do your best.

Mwanasaikolojia Babra wa Malekeni aliwahi fanya tafiti na kuja na majibu yafuatayo

"Watu wengi wanapofikisha miaka 40 au zaidi hugundua kuwa vitu walivyovifanya wakati wakiwa na miaka 18 na kuendelea kwa ajili ya kuimpress watu wanaowazunguka, watu hao hawakuwa wakivijali kabisa".

Mfano wa vitu hivyo ni kuvaa vitu vya thamani, kutumia simu za gharama, Magari makali, kuona aibu kufanya aina ya kazi, kujiunga na chama/kikundi flan.
 
Mimi wanangu nawafundisha kwamba nenda shule lakini isiwe mtumwa wa taaluma bali maarifa, jione umesoma Sana ukaanza kuchagua kazi ,wakati mimi ninanyundo, msumeno drill, randa na mavyeti kibao tu nimepaki huko ndani
Utakufa njaaaa
 
Na ukiwa mtu wakupenda kuonekana smart smart una phone Kali, alafu uwe mtu wa kununua Nguo latest ,
 
Habari za asubuhi familia.

Naandika nikiwa na uchungu sana moyoni lengo ni kuwaasa vijana wenzangu hii kitu Watanionaje ni roho ya shetani yenye lengo la kuzuia maendeleo hasa kwa vijana kuchukua hatua ya kuthubutu fursa mbalimbali zinazokuja mbele yao kwa sababu ya STATUS.

Naandika hili baada ya kumkumbuka swaiba angu mmoja hivi ambae kijijini kwao huko alisoma hadi form six umetusua na wanaamini ukiwa advance unalipwa mshahara hivyo kipindi cha likizo akiwa apeche alolo alikuwa anashindwa kulima vibarua kwa kuogopa watanionaje.

Nawashauri wale wenye Status nendeni mbali na kwenu ndio utajitafuta bila kuangalia pembeni watu wanasemaje.

Nawasilisha
Vijana wanatakiwa wapate ushauriii sanaaa ili waelewe wanatakiwa kufanya nn !la sivyo wata angukia pua hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom