The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limewakamata na kuwashikilia watu watano kwa tuhuma za kupanga njama za kuleta vurugu ikiwemo kuchoma moto vituo vya mafuta, vituo vya mabasi, ofisi za CCM na nyumba za watumishi wa serikali mkoani humo siku ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2025.
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Paulo Chacha wakati wa kikao cha Kamati ya Amani na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, ambapo amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua zingine za kisheria.
RC Chacha amebainisha waliokamatwa kuwa ni Daudi Paulo, Yusuph Jumanne, Warioba, Shabani Swalehe ambao walikuwa wakiongozwa na Abdala Hamadi, na kwamba walikuwa tayari wameandaa madumu ya petroli kwa ajili ya kutekeleza vurugu hizo na kwamba vyombo hivyo vinaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine ambao walikimbia baada ya wenzao kukamatwa.
Hata hivyo, Chacha amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo vilijipanga vyema kuhakikisha usalama kwa wananchi kabla, wakati na baada ya uchaguzi ambapo zoezi hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.