Watanzania 70% hawatumii mitandao ya kijamii hasa vijijini. Wapinzani, wanaharakati katoeni elimu kuhusu katiba na mfumo wa vyama

Watanzania 70% hawatumii mitandao ya kijamii hasa vijijini. Wapinzani, wanaharakati katoeni elimu kuhusu katiba na mfumo wa vyama

Matulanya Mputa

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2023
Posts
245
Reaction score
655
Kuna kasumba moja ya wanasiasa hasa upinzani na wanaharakati wamekua wanaikosoa serikali, au mifumo mibaya ya uongozi, ubovu wa katiba ya sasa kupitia mitandao ya kijamii na makongamano ya wao kwa wao badala ya kuwashirikisha wananchi.

Mf; Unakuta linaendeshwa kongamano la katiba au demokrasia unawaalika viongozi wa kisiasa, wanasheria tena walewale, tena makongamano haya yanafanyika mijini tu tena DSM je wananchi wanapata vipi hizo fursa?

Badala yake mnashindwa kufanya makongamano vijijini ili watu wajue kuna katiba mbovu?

Je, serikali ingesema isijenge shule vijiji au wangejenga shule DAR tu wajinga wangekuwa kiasi gani nchi hii?

Vijiji vingine hayo makongamano, midahalo hiyo hawaijuhi zungukeni nchi nzima wekeni kambi vijiji siyo kuandika tu kwenye mitandao ya kijamii,wakati wananchi wa vijijini hawajuhi hayo mnayoandika.
TLS, TCD zungukeni kutoa elimu vijiji siyo kuitana kwenye mahoteli makubwa na kulipana posho.

Kwa mfumo huu ukiendelea CCM itatawala miaka 1000 watanzania wengi bado wajinga tena ujinga wa sahivi umeota mizizi sasa endeleeni na makongamano kufanyia UDSM, kwenye mahotel makubwa na kutumia online Tv ambazo ata mwananchi wa kijiji hazijuhi.

Leo nakubaliana na Dkt SAMIA raisi wa JM wa Tanzania kuwa MNATAKA KATIBA WAKATI ATA WANANCHI HAWAJUHI KATIBA "kwa hali ya kawaida unaweza omba kitu ambacho hukijuhi, ni aibu tubadilike tuhache siasa za mitandao na tv online tuende vijijini tuweke kambi mkifanya ivi mwaka mtanikumbuka.
 
Back
Top Bottom