Watanzania acheni unafiki, ina maana kifo cha Ivan kimewauma kuliko Dogo Mfaume?

Watanzania acheni unafiki, ina maana kifo cha Ivan kimewauma kuliko Dogo Mfaume?

Kama huna chapa hufariki bali unakufa, na mtu aliyekufa hazungumziwi bali aliyefariki
 
Watanzania kwa unafiki tu hatujambo, sishangai ndio maana hatuendelei.

Leo nimeshangaa sana baada ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii nakuta watu wengi wakilia na kuonyesha kuumia sana na kifo cha Ivan, kwanza niseme tu mimi nilikua simjui huyo ndugu, nikataka kujua ni mtu wa wapi nikaambiwa ni mganda alikua mume wa mke wa Daimondi.

Nikauliza kama ni msanii labda wa muziki au maigizo nikaambiwa hapana ni social celebrity tu, anyway sina shida na hilo lakini kilichonishangaza ni kukuta watu kuonekana wameumia sana na kifo cha Ivan kuliko mtanzania mwenzao Dogo mfaume ambae amezikwa juzi na sikuona msanii yoyote ametupia picha ya dogo mfaume au basi kutoa pole.

Utashangaa kifo cha Ivan kimewaumiza sana watanzania kuliko mtanzania mwenzao aliefariki juzi tu hapa, na utashangaa kujua kua watanzania wameumia sana na kifo cha Ivan kuliko hata waganda.

Unafiki jambo baya sana.


Zaidi ya kuvuta mibange na unga ana mchango upi katika jamii wa kutufanya kupotez bando zetu kumlilia?
 
Unakufa hujaacha Mali za Watu kutoana Ngeu unajiita kweli Mwanaume?
Kama familia yenu imejaa vibaka, watu wasio na shughuli ya kufanya, Losers mnaotegemea ndugu/baba yenu afe mgawane mali poleni sana.

Sisi kwetu ukifa hakuna anaetegemea mali yako, kila mtu ana hela zake za kumtosha kuishi na familia yake.

Tafuta hela yako acha kuzengea ndugu yako/baba yako afe utoane ngeu na ndugu zako.
 
Hatupangiwi wa kumlilia

We endelea kumlilia huyo mfaume wako aliyekufa kwa matumizi ya ngada sisi tuache tumlilie Ivan
Kufa ni kufa tu hakuna kufa kuzuri, alikufa kwa ngada na huyu kama kwa HBP vyote ni vifo tu.

wewe unalilia aina ya kifo au unalia mtu kafa, sitaki kuamini akili yako imefikia hapa, hapana, you are better than this mtanashati.
 
Yile dogo mfaume alikuwa mubuya ngada sasa ss watu wazima nahakilizetu tukajadili mubuya unga.. Ivani tunasikitika kwasababu alikuwa nimti anaejitambua najambo lingine alikua nimtu mwenyeuwezo wakufeza maana alikua namakampuni.. Hatusikitiki sana kwasababu kafatajili bali tunawasilitikia wafanyakaziwake waliopo maana makampuni mengi ya kiafirika anapokufa mwenyekampuni na makampuni yake huishia pale inamaana ajila za wafanyakaziwake ziko lehani.nakwavile watotowake bado niwadogo nawao wanaweza kupigwa changa la macho mali zababayao zikaliwa nawajanja hilo ndilolilo tuhuzunisha
 
Kwani ivan akililiwa inakupunguzia nini wewe. Kwani yeye sio binadamu

Mkuu una wivu hadi kwa marehemu aisee

Jifunze kusoma na kuelewa kabla hujawashwa kujibu, wapi nimesema yeye sio binadam na hatakiwi kuliliwa? Kabl hujakurupuka kujibu jambo lolote jitahidi kwanza kuelewa usije kuonekana mweupe kichwani hata kwa vitu vilivyo wazi kabisa hata mtoto wa chekechea anaweza kuvielewa.
 
Kanisani kwenyewe akifa Kapuku anakuja Katekista tu, hata kama ulikuwa unahudhuria Jumuiya, ngoja afe Bosi Mkurugenzi Kitambi Meneja, hadi askofu utamwona.

Kumbuka Mar Komba mazishi yake, ulizia mara ya mwisho kaenda jumuiya lini.
 
Maisha ya Mwanadamu ni kama maua, ni mafupi sana

Mungu nipe maisha marefu nifurahie mafanikio ya watoto wangu.

RIP ivan
 
Back
Top Bottom