Leo nimesubiri kwa hamu nione nini kimejiri huko jijini Mbeya kwenye mkutano wa CHADEMA, imefika saa 2 usiku nikakaa sebuleni kutizama taarifa ya habari
Kilichonisikitisha taarifa kuu ya mkutano huo ikawa kupokelewa kwa Dr. Slaa, na taarifa ya mkutano huo ikawa imeishia hapo kwamba Azam (UTV) ndio habari kuu wameona hiyo
Hawakutaka hata watazamaji wao wajue ajenda ya mkutano huo ni nini, kwaiyo bila online tv's waTanzania hawawezi kujua chochote kuhusu vyama vya upinzani
Imenifanya niwaze matamko ya baadhi ya viongozi ambayo moja kwa moja yalifaa kufunguliwa kesi za kijinai lkn mpaka leo kimya
Yule bwana mdogo wa UVCCM Kagera alivyodai watu wakipotea polisi wasichukue hatua yoyote kijana mpaka leo yupo mtaani anadunda, kuna yule aliekuwa mkuu wa wilaya Longido aliishia kuachishwa kazi tu lkn mpaka leo yupo mtaani
Kwa hali hii inavyooneka na upendeleo wa wazi wazi kiasi hiki sioni kama kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki
CHADEMA naona wako sawa sana kuja na sera ya no reform, no election wasiwasi wangu ni watafanikiwaje?
Mm kama mwanaCCM bado naamini kwenye ushindani huru na wa uwazi, tuna wanachama wengi kuliko chama chochote nchini, tuna rasilimali fedha kubwa kuliko chama chochote nchini kwanini tuendelee kutoamini kama box huru la kura linaweza kutupa ushindi
Kuna wafanyabiashara kibao mtaani wamechoka na mifumo ya kikodi nchini hawana namna wameamua kuufyata tu maana ukiinua mdomo useme kuna uwezekano kesho uamke na kesi ama ufilisiwe namna pekee ni kuiunga mkono CCM
Tuliombee taifa.