Watanzania hatumtendei haki Vanessa Mdee

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Vanessa mdee ni msanii pekee wa kike wa Tanzania anaefanya vizuri Africa kwa ujumla, ukichukua wasanii 5 wakike bora africa kwa sasa huwezi muacha vanessa mdee hata nominations mbalimbali za tuzo kubwa africa zimethibitisha hilo.

Nimekuwa nikifuatilia kwa muda hasa hapa nyumbani pamoja na uwekezaji wake mkubwa kwenye music wake na kutoa hits kali zinazotamba africa amekuwa hafanyi shows (matamasha) ambazo kiasi kikubwa ndo humuingizia msanii kipato, tunajua mfumo wa kuuza album tanzania haulipi.
Sasa nimekuwa najiuliza kwanini vanessa mdee hafanyi shows kubwa, je Tatizo ni waandaaji? Au mfumo wa mziki wa Tanzania?

Siku moja nilimsikia Vanessa mdee akisema “Kubwa zaidi ni masuala ya bookings msanii wa kike kupewa kile anachostahili, mwanaume atalipwa zaidi siku zote japo msichana ana hit song anaweza kuvuta wale wale atakaovuta
akinakaka,” Vanessa aliiambia 255 ya XXL kupitia
Clouds FM.

Siku kadhaa zilizopita nimeona vanessa akitangaza shows zake nikasikitika sana baada ya kuona mabongo yake



Hivi vanessa mdee kwa ukubwa wake ni wakufanya shows kwenye kumbi ndogo za nights clubs hapa nyumbani? Ukubwa wa vanessa mdee hana tofauti na ukubwa wa diamond platnumz ambeye kimsingi ameshaacha kufanya shows za clubs hapa Nyumbani.

Vassena mdee sasa hivi anapaswa kufanya shows kubwa kwenye viwanja vikubwa kama mlimani city, uwanja wa leaders, na viwanja vya mipira huko mikoani tena shows za kusimama mwenyewe bila kundi la wasanii.
Ni wakati sasa kutambua thamani ya huyu mdada hasa waandaaji wa matamasha.

Shows za clubs, birthday sasa ziwe mwisho.
 
Kila mbuzi hula urefu wa kamba yake.. Nakubaliana na wewe Vanessa yupo juu kwa sasa Baada ya WCB cha ajabu anakomaa na show mara sijui igunga mara sijui vyuon huko iringa.... Lakini kwa upande mwingine anachofanya ni sawa maana anatoa burudan kwa watu wake wote wenye kipato cha chini wasio na uwezo... Yote sawa sema mitazamo tofauti kubwa ni kuwa kama ana kipaji apige kazi ipo siku
 
Mimi si mpenzi wa mziki wa kizazi kipya lakini kwa wakati mchache ninaoangaliaga hii miziki nimegundua kuwa aina ya mziki anaoufanya huyo binti kwa kiasi kikubwa unamtenga na hadhira ya hapa nyumbani kwa kuwa katika mziki anaweka uzungu mwingi mpaka anakuwa kinyaa kama sio kutia kichefu chefu....ni binti mrembo mwenye sauti nzuri sana isipokuwa tu matendo yake afanyapo huo mziki ndio vinavyotia kinyaa kama sio kutapisha kabisa.....

Kwa kila anayemfahamu huyo ni lazima atakubaliana na mimi kuwa vidio ya mziki wa huyo binti huwezi kutazama ukiwa na watu ambao unawaheshimu labda wote muwe wendawazimu au muwe mmelewa.....

Yaani amekuwa hayathamini kabisa maungo yake nyeti....bila ya kusahau na kutuimbia kwa kiingereza ambapo anajua wazi kuwa sisi tulio wengi lugha hiyo ni kitendawili ambapo inakulazima uwe na kamusi ili kuuelewa mziki wake.......

Kwa kifupi huyo binti anatakiwa abadilike na apige mziki wa kinyumbani zaidi ambao unawagusa wananchi moja kwa moja......

Nawasilisha.....
 
Hapo kwenye wenye kipato cha chini hoja yako haijakaa sawa, hivi akiandaa tamasha pale leaders kiingilio kikawa iyo elfu 10,000 hata weza kujaza huo uwanja? Na kukuza brand yake?
 
Uje na suluhisho tufanye nn. Na ni watu gani wa kumfanya vanesa mdee unaemtaka.
 
List wa wasanii wanaofanya vizuri kimataifa
1.Diamond platnumz.
2.Vannesa mdee
3.Navy kenzo
4.Joh makini
5.Ali kiba
Najua Kuna watu watanipinga lkn kama mfuatiliaji mzuri wa station kama mtv, trace na stv rotation ya nyimbo zao ni kubwa. Nirudi kwenye mada husika Vannesa ni msanii mkubwa sana na hata nyimbo yake ya niroge bonge la hiti, ila wanaotuaharibia mziki wetu ni kiba na mondi ambao wameziteka kuanzia media mpaka watangazaji plus mashabiki oya oya hawaoni wala hawambiwi. Ukiangalia nyimbo zilizotoka kipindi hiki Kuna nyimbo kali kuliko Aje lkn hazipati rotation ya kutosha kama NIROGE ya Vannesa, SAMAKI ya Galatone, MOYO MACHINE wa Ben Pol, KUBALI jina la msanii limenitoka ila video wamefanya kwetu studio, ukizitizama hizi nyimbo ni kali sana. Tukitaka mziki wa bongo uwe fair kwanza lazima hii beef na hizi tim zife ndio media na watangazaji watawaona hawa wasanii la sivyo kiba na Dimond hata watoee nyimbo mbaya vipi zinaonekana nzuri tu.
 
Bongo ni rahisi kuwa na jina kubwa lakini hela hauna.

Sasa mnataka ajivunie jina wakati hana hata mia.

Apige shoo tu asake pesa. ..pia apunguze "uzungu"
 
Ni kweli Vanessa ni msanii mkubwa sana Afrika, lakini ninachokiona kwa V. ni kuwa alianza kujulikana zaidi "nje" kabla ya "ndani" sasa wacha aanze pilika za kujitambulisha "ndani" ili aendelee kutoboa vizuri "nje". Na nina amini kuwa hata yeye kalijua hilo ndio maana sasa hivi anatoa nyimbo za kiswahili na anapunguza "uzungu" kiasi japo bado, na anaenda kujitambulisha mikoani. Chakufanya ni kama anavyofanya sasa aendelee kuupunguza kama sio kuumaliza kabisa "uzungu" wake tena hii asiishie kwenye nyimbo kutoa za kiswahili ila pia video apunguze "uzungu" na hata muonekano wake kwenye mitandao na anapokwenda kuhojiwa awe kama mswahili maana hao ndio wateja wake.
 

'''Naomba unirogee''' song la kiswaz kabisa
 
KUBALI imeimbwa na Future Jnl, kama sijakosea
 
ni kweli aina ya mziki wake unatushinda tulio wengi
kajaza uzungu sana ndo maana hatumuelewi ....
 
vanesa aache kujifanya beyonce kwanza aimbe kiswahili nyimbo zenye maana video zake za ajabu ajabu kama za akina lady gaga aache akihojiwa aongee kiswahili ajaribu kuishi maisha ya kawaida kidogo watu watamuelewa maana sisi kina watoto wa uswazi hatumuelewi kabisa alafu pia show zake aache kuruka ruka tunataka kusikia sauti yake kucheza aachie madensa
 
Tatizo la Vanesa muziki wake haujakaa kitanzania na ni ngumu sana kumjua ni Mtanzania (Kiswahili tu ndio identity kuwa ni Mbongo ).Shaa alikuwa hivyo hivyo ikabadilika akatoa Sugua Gaga at least akapata mashabiki huku Uswazi.Na pia anatakiwa kufanya kulabo na wasanii wanaokubalika hapa Tanzania
 
1. Aina ya nyimbo anazoimba (zina uzungu mwingi)

2. Kumbuka Vanessa mdee hana manager, anajiongoza mwenyewe na ushauri kutoka kwa weusi na the industry.. Hii kitu kwa namna moja au nyingine inaweza kuwa inamfelisha huwezi kufananisha na mtu kama Diamond mwenye managers 3 na washauri kibao

3. Hayupo controversial. Msanii kuwa na jina kubwa bila kuwa midomoni na akilini mwa mashabiki muda mwingi ni tatizo, watu wanakuwa hawana muda na wewe hata ukitoa nyimbo mapokezi ya youtube & mkito hayawi makubwa kiivo
Diamond (Mahusiano, tiffah, n.k)
Alikiba (Jokate, bifu na mond, ukaribu na Wema)
Jide (Vimbwanga vya ndoa) n.k
 
Inawezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…