Watanzania hatumtendei haki Vanessa Mdee

Watanzania hatumtendei haki Vanessa Mdee

Mimi si mpenzi wa mziki wa kizazi kipya lakini kwa wakati mchache ninaoangaliaga hii miziki nimegundua kuwa aina ya mziki anaoufanya huyo binti kwa kiasi kikubwa unamtenga na hadhira ya hapa nyumbani kwa kuwa katika mziki anaweka uzungu mwingi mpaka anakuwa kinyaa kama sio kutia kichefu chefu....ni binti mrembo mwenye sauti nzuri sana isipokuwa tu matendo yake afanyapo huo mziki ndio vinavyotia kinyaa kama sio kutapisha kabisa.....

Kwa kila anayemfahamu huyo ni lazima atakubaliana na mimi kuwa vidio ya mziki wa huyo binti huwezi kutazama ukiwa na watu ambao unawaheshimu labda wote muwe wendawazimu au muwe mmelewa.....

Yaani amekuwa hayathamini kabisa maungo yake nyeti....bila ya kusahau na kutuimbia kwa kiingereza ambapo anajua wazi kuwa sisi tulio wengi lugha hiyo ni kitendawili ambapo inakulazima uwe na kamusi ili kuuelewa mziki wake.......

Kwa kifupi huyo binti anatakiwa abadilike na apige mziki wa kinyumbani zaidi ambao unawagusa wananchi moja kwa moja......

Nawasilisha.....
Umesema kweli tupu neno moja uzungu mwingi mno kwa dada etu, binafsi simpendi wala sipendi mziki wake kisa uzungu wake
 
Kinachomfelisha ni uzungu tu hakuna kingine, hakuna msanii aliyewahi kutoboa bongo kwa swaga za kizungu, lazima ajue anadeal na watu gani. Hata bwanaake Jux hawezi kutoboa bongo kwa aina ile ya mziki anayoifanya, na uhakika hata Shilole mziki umemnufaisha kuliko Vannesa, ni kwakuwa mziki wake unaendana na watanzania japo kipaji chake hamfikii hata robo Vannesa. Navy Kenzo na wenyewe walikuwa wazungu sana, ila tangu wametoa kamata chini wamefanikiwa kuturoga wabongo, sahvi wanapiga show kila wiki, abadilike kama anataka kufanikiwa kwny mziki, sio anatoa audio ya kiswazi ila video zimejaa uzungu, ataendelea kusubiri sana
 
List wa wasanii wanaofanya vizuri kimataifa
1.Diamond platnumz.
2.Vannesa mdee
3.Navy kenzo
4.Joh makini
5.Ali kiba
Najua Kuna watu watanipinga lkn kama mfuatiliaji mzuri wa station kama mtv, trace na stv rotation ya nyimbo zao ni kubwa. Nirudi kwenye mada husika Vannesa ni msanii mkubwa sana na hata nyimbo yake ya niroge bonge la hiti, ila wanaotuaharibia mziki wetu ni kiba na mondi ambao wameziteka kuanzia media mpaka watangazaji plus mashabiki oya oya hawaoni wala hawambiwi. Ukiangalia nyimbo zilizotoka kipindi hiki Kuna nyimbo kali kuliko Aje lkn hazipati rotation ya kutosha kama NIROGE ya Vannesa, SAMAKI ya Galatone, MOYO MACHINE wa Ben Pol, KUBALI jina la msanii limenitoka ila video wamefanya kwetu studio, ukizitizama hizi nyimbo ni kali sana. Tukitaka mziki wa bongo uwe fair kwanza lazima hii beef na hizi tim zife ndio media na watangazaji watawaona hawa wasanii la sivyo kiba na Dimond hata watoee nyimbo mbaya vipi zinaonekana nzuri tu.
Hiyo list ni ya kweli
 
Umesema kweli tupu neno moja uzungu mwingi mno kwa dada etu, binafsi simpendi wala sipendi mziki wake kisa uzungu wake
...acha unafki!...username yako tu ya kizungu!...JF na devices unazotumia za kizungu!..sijui kama bado wavaa magome ya miti siku hizi!
 
WCB ya Diamond Platnumz gonna be some fucking TIDAL ya Jay Z , ili utoke na uwe msanii mkubwa na u maintain climax yako ni lazima ujiunge nao....

Vaness mdee hajui soko lina taka nini, na mashoga sake wengi wa mujini wanao mpa bichwa na kumfariji kua Ana u Beyonce flani au ua Ariana grande ndani yake...

100% guarantee shilole is way better kuliko Vanessa, ni vile ngeli kwake imekua tabu, na management pia hana inayo weza kum expose nje ya inchi na kumkutanisha na artists wengine.

Nyimbo za Vanessa tuta zisikiliza chumbani tu tukiwa na ma demu zetu...
 
Mimi si mpenzi wa mziki wa kizazi kipya lakini kwa wakati mchache ninaoangaliaga hii miziki nimegundua kuwa aina ya mziki anaoufanya huyo binti kwa kiasi kikubwa unamtenga na hadhira ya hapa nyumbani kwa kuwa katika mziki anaweka uzungu mwingi mpaka anakuwa kinyaa kama sio kutia kichefu chefu....ni binti mrembo mwenye sauti nzuri sana isipokuwa tu matendo yake afanyapo huo mziki ndio vinavyotia kinyaa kama sio kutapisha kabisa.....

Kwa kila anayemfahamu huyo ni lazima atakubaliana na mimi kuwa vidio ya mziki wa huyo binti huwezi kutazama ukiwa na watu ambao unawaheshimu labda wote muwe wendawazimu au muwe mmelewa.....

Yaani amekuwa hayathamini kabisa maungo yake nyeti....bila ya kusahau na kutuimbia kwa kiingereza ambapo anajua wazi kuwa sisi tulio wengi lugha hiyo ni kitendawili ambapo inakulazima uwe na kamusi ili kuuelewa mziki wake.......

Kwa kifupi huyo binti anatakiwa abadilike na apige mziki wa kinyumbani zaidi ambao unawagusa wananchi moja kwa moja......

Nawasilisha.....
mziki hauna lugha jamaa
 
wabongo bwana, mi naona tangu SHAA kaamua kuimba kiswazi Swazi kapotea kabisa tofauti alivyokuwa anapiga swaga za kizungu alikuwa anaosha sana ma MTV , channel 0 n.k ..Lazima tuwe na miziki aina tofauti wengine wapige singeli, wengine baikoko,taarabu , miduara, chura style na miziki ya kishua nayo lazima iwepo maana si wote tunaishi huko ushenzini kucheza miziki ya kuvaa madera. Ana miaka miwili kwenye game atapanda taratibu Kwa wakati wake msitake kumrusha ghafla afanane na wakongwe kina diamond na Alikiba or jide
 
Mwanamke aliyejiremba ivo huwa hanipi msisimko.
Nahisi akienda kuoga au mvua ikinyesha kila kitu kitapukutika.
 
Kazi yake ni kuimba na atuimbie tu popote tulipo
 
...acha unafki!...username yako tu ya kizungu!...JF na devices unazotumia za kizungu!..sijui kama bado wavaa magome ya miti siku hizi!
Wewe mzungu kamsapoti vanessa mimi simsapoti maishaa yangu hadi abadilikee huo uzungu wake hutaki acha
 
mziki hauna lugha jamaa

Lakini una mahadhi na asili kutoka na mahali na hadhira husika.....ndio maana kila jamii ina aina ya mziki wake unaowatofautisha na jamii zingine......
Ukipigwa mziki wenye asili ya Caribean kila mtu atajua....
Ukipigwa mziki wenye mahadhi ya kiNigeria kila mtu atafahamu.......hata hao wasanii wa africa magharibi wanatamba ulimwenguni kwa kupiga miziki yenye asili yao kuanzia ala za muziki mpaka aina ya uimbaji.....
Lakini unapojaribu kuuleta aina ya mziki mpya kwenye jamii ambayo tayari kuna aina ya muziki imeshaipokea na kuufurahia lazima muitikio wa mziki huo uwe mdogo kwenye jamii hiyo....
 
Hana good pr... Halafu amejikoboa koboa and full of stuffs in her body hadi kawa kama shetani

She has really disappointed
 
Wewe mzungu kamsapoti vanessa mimi simsapoti maishaa yangu hadi abadilikee huo uzungu wake hutaki acha
...kituko!...unamtaka abadilike aache 'uzungu' wake ndio uumsapoti wakati wewe bado waitwa john agrey!?
....huna hoja zaidi ya unafki!
...ushauri ukurudie na wewe;humtaki,MUACHE!
 
Back
Top Bottom