Watanzania hawachukii ufisadi bali humuonea wivu anayekula

Watanzania hawachukii ufisadi bali humuonea wivu anayekula

Mishenyi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2019
Posts
464
Reaction score
748
Watanzania hawachukii ufisadi na ukiona wanapiga kelele ujue ni wivu tu kwa mtu fulani, ukitaka kujua hilo mtafute mpiga kelele mmoja mpe nafasi uone maajabu!

Mtanzania na wizi ni mtu na Nduguye hawatengani, watz ndivyo tulivyo. Ni wezi hakuna mzalendo hata sisi tunaopiga kelele tunahitaji tu nafasi tupige. Tukipata nafasi hutatusikia tena!

CCM imetengeneza hilo kuwa kama mfumo wa nchi yaani "Piga kelele kama hujapata ukipata Nyamaza".
 
Upo sahihi kabisa ndio maana mtu akiteuliwa nafasi ya kutumika taifa tunasema 'ameula', 'ametusua' au 'amepata shavu'.
Naaam umenena!! Hayo ndo maneno yetu wtz yaani tupo hovyo hakuna mwenye afadhali!!! Ni wezi mpaka mungu anachukia
 
umewaza kama taahira, si kila mtu ana hulka ya tamaa, kuna watu huko ndani ya system hua hawachukui hiyo migao ya pesa haram japo hukosa tu uwezo wa kuzuia.
 
Likely true
Kwenye mojawapo ya kesi fulani ya miaka ya nyuma ya maswala ya fedha za Serikali kuchotwa kinyemela, nilijaribu kufanya utafiti wa juu juu kuhusinana na watu waliokuwa wanalalamika kuhusiana na fedha hizo kupotea.

Nilichokuja kubaini ni kuwa wachache sana walikuwa wameumizwa na issue nzima ya hela hizo za umma kupotea, lakini wengi wao malalmiko yao yalikuwa yamejikita katika kulalamikia issue nzima ya kwa nini zilipita kwenye mikono ya makanyaga na siyo kwenye mikono yao wenyewe.

Yaani walikuwa wanalalamika kwa sababu walitamani ziwe zimepita kwenye mikono yao walalamikaji hao
 
umewaza kama taahira, si kila mtu ana hulka ya tamaa, kuna watu huko ndani ya system hua hawachukui hiyo migao ya pesa haram japo hukosa tu uwezo wa kuzuia.
We ndo taahira kabisa ukiona mtu kakaa kimya ujue kalambishwa kitu tyr!!! Kama mzalendo kwanini asipaze sauti kwa kutoa ushahidi usiobakiza shaka!!!?
 
... hiyo ni hulka ya binadamu sio watanzania tu; duniani kote binadamu ni wabinafsi sana. Kwa kutambua hulka hiyo ya kibinadamu; nchi zenye watu wenye akili huhakikisha wanaweka miundo ya kuwadhibiti wenye nafasi za kula ili wasile wakavimbiwa; tena imeandikwa "toshekeni na mishahara yenu". Kutoatoa vitamko vya "kuwakanya" walafi bila kuwa na strict measures hasaidii; binadamu ni viumbe wa ajabu. Nchi kama China wana measures zao tena ni kali kweli kweli.

... sisi sio lazima tufuate njia ya China au kwingineko wenye adhabu kali; bali tuanze kuboresha sheria mama - Katiba. Baadhi ya wenzetu hawataki kuona hilo linatokea; kwanini? Kwa sababu Katiba ilyopo inawahakikishia kufaya ufisadi bila bugudha; na hata akiingia mwingine kwa Katiba hii huenda akawa fisadi haswa! Katiba Mpya ni hatua muhimu ya kuanza nayo.
 
umewaza kama taahira, si kila mtu ana hulka ya tamaa, kuna watu huko ndani ya system hua hawachukui hiyo migao ya pesa haram japo hukosa tu uwezo wa kuzuia.
We ndo taahira kabisa ukiona mtu kakaa kimya ujue kalambishwa kitu tyr!!! Kama mzalendo kwanini asipaze sauti kwa kutoa ushahidi usiobakiza shaka!!!?
 
Naunga mkono hoja...wapinga ufisadi ndio mafisadi wenyewe hawajapati mfereji tu...

Jitu linawasema wenzie au wezi wa serikalini wakati lenyewe kutwa kucha linadhurumu watu mtaani huku, linanunua vitu vya wizi,limission town, lijizi, linashangilia mafanikio ya mjomba ambaye ni fisadi serikalini tena na ada ya watoto linasaidiwa kulipiwa...

Tungekuwa wote tunauchukia ufisadi kwa dhati hapa Tanzania either usingekuwepo au ungekuwa negligible...
 
Back
Top Bottom