- Thread starter
- #21
Kwahiyo sisi ni wadhaifu kiasi hadi tushindwe kutengeneza mifumo!??? Hadi aje mzungu atengeneze!?... hiyo ni hulka ya binadamu sio watanzania tu; duniani kote binadamu ni wabinafsi sana. Kwa kutambua hulka hiyo ya kibinadamu; nchi zenye watu wenye akili huhakikisha wanaweka miundo ya kuwadhibiti wenye nafasi za kula ili wasile wakavimbiwa; tena imeandikwa "toshekeni na mishahara yenu". Kutoatoa vitamko vya "kuwakanya" walafi bila kuwa na strict measures hasaidii; binadamu ni viumbe wa ajabu. Nchi kama China wana measures zao tena ni kali kweli kweli.
... sisi sio lazima tufuate njia ya China au kwingineko wenye adhabu kali; bali tuanze kuboresha sheria mama - Katiba. Baadhi ya wenzetu hawataki kuona hilo linatokea; kwanini? Kwa sababu Katiba ilyopo inawahakikishia kufaya ufisadi bila bugudha; na hata akiingia mwingine kwa Katiba hii huenda akawa fisadi haswa! Katiba Mpya ni hatua muhimu ya kuanza nayo.