Watanzania hawachukii ufisadi bali humuonea wivu anayekula

Kwahiyo sisi ni wadhaifu kiasi hadi tushindwe kutengeneza mifumo!??? Hadi aje mzungu atengeneze!?
 
Braza natamani nikupe zawadi sema ndo hivo january hii sina kitu
 
Kwanini wasiandamane kudai sheria kali za kulinda mali zao badala yake wako kama mazombi!! Wanasubiri na wao waingie kwenye mrija wa kula sheria hizo hizo dhaifu ziwalinde!!! Wtz ni wezi sana
Sijui kwanini hawaandamani, ila ninachotaka kujua kuhusu hoja yako, ni kwamba mtu akiibiwa halafu akamchukia aliyemuibia, ni wivu? Sio?
 
Kwa hii Post Unakuwa umewakosea sana Heshima.watu waliotumikia hili taifa kwa uaminifu na bila kuiba ingwaje walikuwa kwenye nafasi za kufanya uovu huo. Kila mtumishi angekuwa fisadi kama hao mnaowapigia chapuo, hii nchi ingekuwa ya mwisho duniani. Isinge sogea hata hizi hatua tulizopiga. Usingeona hizi huduma zikisogea mpaka pale kijijini kwako. Amini kuwa kuna Wazalendo kindakindaki wa hili taifa wanaolipigania kila siku, wengine hata kuuwawa na hao mnaowapigia chapuo wasizomewe. Na Hoa wazalendo wa namna hiyo wameamua kukaa kimya kwakuwa kila wanapofungua mdomo, hugeukwa na watu kama nyinyi ulioandika post hii na kusema wana wivu ama wamekosa. #Wazalendo wa Taifa Hili wapo.
 
Ukweli mchungu,ndio maana na wao wakipata watafanya vilevile.

Afu huwa wanaona mtu akiwa kiongozi ni Halali kufanya ufisadi na upendeleo eti Kisa ni kiongozi na kasoma.

Huonaga hata mtu ana biashara nzuri ila utasikia napata shida kwa sababu sikusoma na kudhirisha hilo anapeleka watoto wake shule wasome na hawafundishi biashara.

Akimaliza akipata Kazi utasikia mwanangu kaajiriwa sehemu x and y na anajiskia fahari bila kujua kwamba kioato cha mwajiriwa ni kidogo Sana yaani biashara yake ni kubwa mmno.

Nadhani shida ni kuona biashara hazina security na yeye mwenyewe kuweka security kwa njia ya michango ya pension toka akianza.biashara.
 
Ni wivu ndy!!! Maana mlalamikaji nae akipata nafasi anakuwa mwizi vile vile!! Mtanzania ni mwizi sana
Sawa, wacha tuendelee kuwaonea wivu wanaotuibia, hata huko mtaani mwizi akikuibia usipate hasira na chuki kiasi mkaanza kumpiga, we muonee tu wivu huku ukimuacha anaondoka zake, maana huwezi kupiga mtu kisa unamuonea wivu
 
Ujue zamani nilikuaga mzalendo Sana ila baada ya kuwagundua jamii ya Tzn ilivyo nikasema kumbe ngoja nijipimie kwa urefu wa kamba yangu.

Tena jamii yetu ninya hovyo Sana ndio maana hata wakiona mgeni hakuna wa kustuka wala kumuuliza yaani hulka ya ubinafsi na kutojali wengine.

Hili ni tatizo la jamii yetu.
 
We ndo taahira kabisa ukiona mtu kakaa kimya ujue kalambishwa kitu tyr!!! Kama mzalendo kwanini asipaze sauti kwa kutoa ushahidi usiobakiza shaka!!!?
hatuwezi elewana coz hujawah fanya kazi yoyote serikalini, kuna watu ni waadilifu/wachamungu ukimambia habari ya dili hamuelewani kabisa, watu hawa hua wanakaa kimya kuepuka kufanyiwa fitna na watu wa madili bt wao hua hawachukui hata sent.
 
hatuwezi elewana coz hujawah fanya kazi yoyote serikalini, kuna watu ni waadilifu/wachamungu ukimambia habari ya dili hamuelewani kabisa, watu hawa hua wanakaa kimya kuepuka kufanyiwa fitna na watu wa madili bt wao hua hawachukui hata sent.
Hao ni maofisa wa chini wasio na access ya kupata pesa nje ya salary na posho zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…