Watanzania hawachukii ufisadi bali humuonea wivu anayekula

Ili ni kweli kabisa.
Hili ni tatizo kabisa.
Mtza kwa pesa za upigaji afai kabisa.
Unakamatwa na rushwa unatoa rushwa kesi inatupwa.
Ni nadra kukuta akufatiliaye eti umekwapua nae ukamp mgao wake akaendelea kukufatilia.
 
Sheria za Tza hazina uwezo wa kumfunga fisadi.Bali vibaka wadokozi.
Wadokozi upigwa miaka mingi fisadi afungwi ulipa faini kiduchu au miaka michache jela.
 
Kweli kabisa kwenye hilo ni kama sote tupo sawa ila sasa utofauti unakuja hapa..

Kuna wale wezi ambao huiba kwa akili na wasistukiwe na wananchi (kama mimi endapo nitapata nafasi) , na pia kuna wale wezi wa waziwazi, watumia mabavu pasipohitajika, wanyang'anyi na mostly hawatumii akili (sabaya, bashite nk nk.)
 
Watza wengi ni wezi.uiba ofisini uleta nyumbani,kina mama uachiwa pesa za chakula uwalisha watoto viporo nao ubana wanatuma kwao na kucheza vikoba,dada wa Kazi nao uzidisha bei ya vitu wakitumwa dukani sokoni.
Maadamu KILA mtu mwizi sio raisi sio mkuu sijui wa nn sio mfagizi KILA mmoja ula urefu wa kamba yake.
Mzungu kutengeneza control number lakini haijamzuia mswahili kuiba.
 
Hawa chawa walijua baba yao ataishi milele wakaamua kuwatenda watz.
 
Hapa kwenye upigaji ishu sio katiba ni tabia yetu halisi.
Watz wengi wamewapiga wawekezaji unawajua wale mapapaa wa mjini Magufuli aliwapukutusha wote wengine wakakimbia nje kina papa msofe,jack pemba nk ni wapigaji wa kimataifa.
China au ulaya ukifanya ufisadi umepotea sheria zao ni kali.
Kama makengeza anatamba wa kumkamata wapo wa kumfunga hayupo si kaona udhaifu wa sheria zetu, thus KILA dili kubwa yupo hadi ukawepo msemo ukitaka kupiga dili kubwa piga na chenge utakuwa salama.
 
... tabia ni lazima ziwe na namna ya kuzidhibiti zisivuke mipaka iliyokubalika katika jamii. Tool ya kudhibiti tabia kiserikali ni sheria na Katiba ni sheria mama.
 
Na ni nini kinakwamisha wote wasile labda.......au umehalalisha wengine kufa njaa.
 
... tabia ni lazima ziwe na namna ya kuzidhibiti zisivuke mipaka iliyokubalika katika jamii. Tool ya kudhibiti tabia kiserikali ni sheria na Katiba ni sheria mama.
Walinda sheria ndio wavunja sheria tutawajibisha vipi walinde sheria!
 
Mungu awapiganie kama wapo!!!
 
Sawa, wacha tuendelee kuwaonea wivu wanaotuibia, hata huko mtaani mwizi akikuibia usipate hasira na chuki kiasi mkaanza kumpiga, we muonee tu wivu huku ukimuacha anaondoka zake, maana huwezi kupiga mtu kisa unamuonea wivu
Sasa kama wewe tabia zako ni mwizi kwanini umsulubu mwizi mwenzio!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…